Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa akigonga
nyundo maalum kuashiria kukamilika kwa Mikutano ya Baraza hilo ambalo
ameliongoza kwa mwaka mzima. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon akiwa mwenye furaha wakati wa kuhitimishwa Baraza
la 69 ambapo alimpongeza Bw. Sam Kutesa kwa kuliongoza Baraza kwa
uhodari uliopelekea kupitishwa kwa maazimio mbalimbali.
Na Mwandishi Maaalum
New York
Mkutano
wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, uliokuwa chini ya urais wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Bw, Sam Kutesa umefikia ukingoni siku ya jumatatu kwa kupitisha maamuzi ya kihistoria ambayo pamoja na mambo mengine
yanatoa mwelekeo wa majadiliano kuhusu marekebisho na mageuzi ya Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa.
Maamuzi
hayo ambayo kwa mara ya kwanza yanaingizwa rasmi katika nyaraka muhimu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na yaliyopewa namba A/69/L.92 yalipitishwa
kwa kauli moja na wajumbe kutoka nchi 193 wanaounda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Maamuzi
hayo ambayo baadhi ya wazungumzaji waliyapachika jina kama maamuzi ya Kutessa ikiwa ni ishara
ya kutambua mchango wake katika kusimamia kidete majadiliano kuhusu mageuzi ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa yanatoa msingi
au maandishi ambayo kwayo yatawawezesha nchi wanachama kujadiliana
kwa kupitia maamuzi hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...