Kuishi kwingi kuona mengi ! katika hali ya utata juzi kati wageni waliokwenda kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mwanamuziki mahili na kiongozi wa Ngoma Africa band a.k.a FFU Ughaibuni kamanda Ras Makunja kule ujerumani walijikuta wakitimuliwa mbio na mlinzi namba one Koplo Dog Domo Baya (pichani) wa Kamanda huyo.
Mbwa huyo aliyechoka lawama za boss wake kuwa amekuwa mzembe kazini , siku ya jumamosi 19 Septemba 2015 majira ya saa 2.00 usiku aliamua kupiga doria ndani ya makao ya himaya Kamanda Ras Makunja, na kila mgeni aliyegusa au kukaribia geti alibwakiwa na kutemewa kibesi na mbwa huyo.
Timbwili hilo lilichukua muda masaa mawili bila kibosile kamanda Ras Makunja kujua kinachoendelea nje ya nyumba,kwani alikuwa ndani na familia yake. dipo mmoja wa watu wake wa karibu alipomtumia ujumbe wa simu asitegemee wageni mbwa kachomoka ndani ya banda na kupiga doria ! baadhi ya marafiki wanamlalamikia Koplo Dog Domo baya kuwa anachagua watu wa kuwatimua... mbwa huyo anawajua wanamuziki wa Ngoma Africa band aka FFU.. tu. Lakini wa wageni wengine yeye kazi ni moja tuu.
Kwanza Ras Makunja kaamua kumtungia songi Koplo Dog Domo Baya, kisha akaamua Kumagufulika ili apambane naye akileta za kuleta. Kamanda kachachamaa
Baada ya kutunga wimbo wa Koplo Dog Domo Baya, Kamanda wa FFU Ughaibuni akaamua Kumagufulika ili isiwe taabu pindi akitaka kutoa adhabu...
mkuu kamanda bora tizi la Magufulika kuliko mlinzi wako Dog Domo Baya
ReplyDelete