Wapendwa wana-Simba wenzangu,
Ninawaandikia ujumbe huu makhsus kuwashukuru kwa mara nyingine kwa kazi nzuri mliyoifanya uwanjani Leo kwa kuishangilia timu yenu mwanzo mwisho kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Taita.
Mimi  naamini bila ya support yenu Simba haiwezi kufanya vizuri hata siku moja.


Pia kwa niaba ya uongozi wenu tunawashkuru sana wapenzi wetu ambao  hawakujaaliwa kufika uwanjani hii leo. Sisi tunaamini dua na sala zao zmesaidia kutupa nguvu hii leo na kupata points tatu muhimu.
Na kwa umuhimu wa pekee tuwapongeze sana wachezaji wetu na bench la ufundi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutupa furaha.hakika hiki ndio wanasimba wanachotaka
Mwisho niwaombe sana.sote wiki hii tuwekeze akili yetu tarehe 26 yaan wiki ijayo.mnajua tuna mechi ngumu dhidi ya watani zetu. Kwa upande wa uongozi umejipanga kwa kila hali kuhakikisha tunashinda game hyo.iwe jua.iwe mvua yanga hawatoki Taifa Jumamosi ijayo.
Wapenzi wetu, tunawaomba sana umoja na mshikamano wenu kuelekea game ya Jumamosi.
Kila mmoja ruksa kufanya awezacho kuhakikisha tunawalaza tena mapema vibonde wetu.Narudia RUKSA.
Mwisho ingawa si  kwa umuhimu niwashukuru wanahabari wote kwa kazi nzuri waifanyayo ya kutuhabarisha habari za mnyama.

Reclaiming our glory
Simba nguvu moja

Imeandikwa na mtumishi wenu
Haji S.Manara

Msemaji wa SSC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal Heading hyo .. MSUMAJI nafikiri badala ya Msemaji (Afisa Habari wa Simba)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...