Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda
kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote
cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge,
urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama
wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live
Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya
utangazaji.
Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui)
(Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h),
(i), 5(b), (d), (e) and (f).
Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka
utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..
IMETOLEWA
NA:
Mkurugenzi
Mkuu
MAMLAKA
YA MAWASILIANO TANZANIA
Tarehe
11/09/2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...