Na Mwandishi Maalum, New York 
Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA) ni kati ya Asasi 21 ambazo jana ( jumatatu) zimetangawa kuwa washindi wa Tuzo ya Ikweta (Equator Prize ) kwa mwaka 2015 Tuzo hiyo ya Ikwete hutolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofadhili tuzo hiyo. 
Kila NGO iliyoshinda Tuzo hiyo inanyakua kitita cha dola 10,000 za Kimarekani. Ushindi wa MJUMITA pamoja na NGO nyingine 20 ulitangazwa na Mkuu wa UNDP Bi. Helen Clark katika mkutano wake na wawakilishi wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa Wawakilishi wa NGO hizo 21 watapokea Tuzo zao mwezi Desemba wakati wa Mkutano wa Kimataifa utakaojadili mabadiliko ya Tabia nchi ( COP21) utakofanyika Paris, Ufaransa. 
MJUMITA ni mtandano wenye wanachama katika vijiji 450 vilivyopo katika Wilaya 23 za Tanzania na hujishughulisha na utunzaji wa misitu, kuwasaidia wanavijiji kupata hati za kimila za kumiliki ardhi, kutatua migogoro inayohusisha masuala ya ardhi na kubuni miradi ya matumizi sahihi ya ardhi pamoja na raslimali za misitu. 
 Zaidi ya watu 500,000 wamenufaika na huduma zinazotolewa na MJUMITA Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi hao Bi Helen Clark, aliyefuatana na Bi. Christiana Figueres anayeshughulika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Bw. Alec Baldwin ambaye ni mcheza sinema maarufu na mwanaharakati wa mazingira. 
 Amesema kuwa NGO hizo ambazo zinajihusisha Zaidi na utunzaji wa mazingira, kupambana na umaskini , utunzaji wa ardhi na matumizi endelevu ya ardhi na misitu wamedhihirisha kwamba wanalo jambo la kuifundisha Jumuiya ya Kimataifa. 
 Akaongeza kwamba Zaidi ya washiriki 100 waliingia katika shindano hilo lakini 21 ndio walioibuka kidedea, huku akisisitiza kila NGO ilizoibuka mshindi ina hadithi ya aina yake yenye funzo Jumuiya ya Kimataifa Akasema kupitia kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kijamii pasipo kutumia gharama kubwa au teknolojia za hali ya juu imedhihirika kwamba kuna juhudi ambazo zinatoa matokeo na watu wengi hasa maskini wanasaidia na hali yao ya maisha inaboreka na maliasili ikiwamo misitu na ardhi.Mbadiliko ya Tabia nchi ( COP21) MJUMITA ni kati ya NGO Sita kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, zilizojinyakulia tuzo hiyo. NGO nyingine zilizoshinda Tuzo Nane zinatoka Asia na Pacific na NGO nyingine Nane ni kutoka Latin Amerika na Visiwa vya Karibbean.
Bi. Helen Clark, Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo  wa Umoja wa Mataifa ( UNDP)  akiwatangaza washindi wa Tuzo ya Ikweta ambayo hutolewa na Umoja Mataifa kwa  NGO ambazo zinajihusisha na utunzaji wa  mazingira, ulinzi na uhifadhi wa misitu, matumizi bora na endelevu ya ardhi na mali asili na  kupiga vita umaskini. Tuzo ya mwaka huu wa 2015 ambayo ni  dola  za kimarekani 10, 000 kwa kila mshindi inakwenda kwa NGO 21 ambapo  NGO ya Tanzania ijulikanayo kama Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania ( MJUMITA) ni kati ya NGO sita kutoka Afrika  Kusini  mwa Jangwa la Sahara zilizoshinda Tuzo hiyo. wengine katika picha ni Bi. Christiana Figueres ( UNFCCC) Mcheza  senema  maarufu na mwanaharakati wa Mazingira Bw.  Alec Baldwin na Mkewe Bi. Hilaria Thomas na Bw. Hans Brattsker ambaye ni Mshauri wa UNDP kuhusu wazawa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni jambo jema, la kupongezwa na la kuungwa mkono kwa wadau wote wapenda mazingira kwa shirika la Mjumita kupata tuzo hiyo ya kimataifa. Hii inadhihirisha kuwa mchango wa Mjumita katika jamii unatambuliwa na kuheshimiwa na wadau wote. Hongereni sana Mjumita!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...