Na Mwandishi Wetu

BONDIA Said Mbelwa anatarajia kupanda uringoni kwa mara nyingine tena kugombania mkanda wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa PST dhidi ya bondia George Dimoso mpambano .
Mpambano utakaofanyika Septemba 26 katika ukumbi wa Butihama Villa Club uliopo chanika mpambano huo wa raundi kumi ulioratibiwa na 
Kocha wa kimataifa nchini Rajabu Mhamila 'Super D' utakuwa ni wa kumaliza ubishi baada ya mpambano wa kwanza Dimoso kudundwa kwa point

Super D aliongeza kuwa siku iyo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali itakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini ambapo 

bondia Seleman Zugo atapambana na Abdallah Ruwanje na Adam Ngange atakabiliana na Shabani Mtengela na Said Uwezo atapambana na Hassan Mgosi uku Hamza Mchanjo ataoneshana kazi na Ally Maiyo mipambano yote ya utangulizi ni ya raindi sita

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...