Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bwana Michael Mhando akizungumza na wafanyabiashara wa wasamaki katika Soko la feri hawapo pichani juu ya vikundi vya wajasiliamali wadogo na wakubwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bwana Michael Mhando akimkabidhi kadi ya uanachama ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mvuvi wa Samaki wa Soko Kuu la Feri Bwana Mohamed Ally Masoud mwishoni mwa wiki Jijini Dara es Salaam.
MFUKO wa Taifa wa
Bima ya Afya NHIF leo umekabidhi bima ya
Afya kwa Wavi wadogowadogo (UWAWADA) wa mkoa wa Dar es Salaam,na Kaimu
Mkurugenzi wa mfuko huo,Michael Mhando .
Mhando amekabidhi Bima hizo leo kwenye soko kuu la kuuzia
samaki Jijini Dar es Salaam maarufu ‘soko la feri’ ambapo awali ua kukabidhi
bima hizo alisema kuwa anawapongeza wanachama wote wa uwawada waliojikusanya
kwa vikundi vya watu kumi na kuhitaji siku ya leo kukabidhiwa Bima zao za NHIF
kwa wanachama 10 waliojiunga na mfuko huo.
Alisema wanachama hao baada ya kukaa na kusikiliza huduma
zinazotolewa na shirika hilo, namna ambavyo wamefanikiwa kufikia hatua hiyo ya
kukabidhiwa bima zao kupitia mpango wa KIKOA ambao unawalenga hasa
wajasiliamali wadogowadogo.
Aidha alisema kuwa vikundi husika kujiunga na mfuko huo
,hunufaika na mafao ya matibabu
sawa na wanachama wanaochangia kupitia mishahara yao ya kila
mwezi.
Mhando alisisitiza kuwa lengo kubwa la mpango wa Mfuko wa
Taifa wa Biama ya Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na
wakubwa ili kuwajumuisha katika mpango huo.
”Lengo letu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni
kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuweza kuwajumuisha
katika mpango huu”alisema Mhando.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...