Kipa
wa timu ya soka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akichupa kuzuia
mpira wa penati bila mafanikio wakati timu hiyo ilipomenyana na ile ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wakati
wa bonanza la pamoja la taasisi hizo mbili lililoandaliwa na PPF na kufanyika
kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam
leo Septemba 5, 2015. Katika bonanza hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi
wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, zawadi
mbalimbali zilitolewa kwa washindi wa michezo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku,
mbio za magunia, soka na mpira wa wavu. (Volleyball)
NA
K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wamefanya bonanza
la michezo kwenye uwanja wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam, leo Septemba 5, 2015 ili kuonyesha ushirikiano.
Akizungumza
kwenye bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa
PPF, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, amesema, bonanza hilo
limewakutanisha pamoja wafanyakazi wa taasisi hizo mbili za umma, ili kuonyesha
mshikamano na ushirikiano sio tu katika Nyanja ya kazi bali pia katika Nyanja
ya michezo na burudani.
Bonanza
hilo lilishirikisha michezo ya kuvuta kamba, soka, mpira wa wafu (Volleyball),
mbio za magunia, na kufukuza kuku, ambapo washindi walijinyakulia zawadi
mbalimbali. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Mazoezi ya viongo kwa wote
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...