Mtaalamu kutoka
Kitengo cha Leseni cha Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani, akiwasilisha
mada kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni wilayani Kahama, kuhusu mfumo
mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo
imefanyika Septemba 11, 2015 mjini Kahama ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo
yanayotolewa na Wizara husika kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za
madini nchini kote.
Na
Veronica Simba - Kahama
Serikali imesema
wachimbaji wadogo wa madini wanaruhusiwa kumiliki idadi yoyote ya leseni za
madini ilimradi waweze kuzifanyia kazi.
Hayo yamesemwa leo
Septemba 11, 2015 mjini Kahama na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Kitengo cha Leseni, Mhandisi Nuru Shabani wakati akiwasilisha mada kwa
wachimbaji wadogo wa madini kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa utoaji leseni za
madini kwa njia ya mtandao, wakati wa semina iliyofanyika mjini humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...