Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wajane na kusaidia watoto,Utti Mwang’amba akizungumza na waandishi habari juu ya  serikali ya awamu ya tano kurekebisha sheria ya kifo kwa makundi maalum iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Pamoja na wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo  leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
TAASISI  ya Children Education Society (CHESO) imeitaka serikali ya awamu ya tano kurekebisha sheria ya adhabu ya kifo  ili kulinda makundi maalum wakiwamo watoto na akina mama wajawazito.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Richard Shilamba amesema Serikali ya awamu ya tano wanaiomba kuondoa adhabu ya kifo katika makundi maalum kutokana na kuwa na mahitaji maalumu.

Amesema makundi hayo wakiwemo akina mama wanaonyonyesha watoto, watu wenye ugonjwa wa akili, pamoja na wazee na badala yake watafutiwe adhabu nyingine.

Shilamba amesema nchi mbalimbali ikiwemo Marekani zimeweza kufuta sheria ya adhabu ya kifo katika makundi maalum na kufanya hivyo hakujaweza kuadhiri masuala yote ya sheria.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa wajane na kusaidia watoto,Utti Mwang’amba amesema wanawake wajawazito akifungwa na kutambua maisha yake ni kifo kinaweza kuadhiri ujauzito wake hivyo kwa wanawake wa jamii hiyo wanaweza kubadilisha adhabu nyingine na sio ya kutumikia kifungo kisicho na ukomo.

Katibu Mtendaji wa Kisarawe  wa Taasisi Paralegals Organisation, Halima Sasi amesema kuna wajibu wa kuangalia sheria ya watoto, makosa yenye adhabu ya kifo.

Halima ameiomba serikali ya awamu ya tano kurekebisha sheria kuangalia sheria ya kumuwezesha mtoto wa makosa ya mauaji kesi yake kuendeshwa katika mahakama za watoto .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi NGO's zinatumiwa kusambaza ajenda za wazungu tu. Adhabu ya kifo iondolewe mbona hawaongelei haki za marehemu ama familia yake. Mtu kaua ushahidi upo, basi. Sisi wengine tuna ndugu wamepoteza maisha kwa makusudi kabisa ya watu waliotaka fedha yake aliyoitolea jasho. Ushahidi upo na hakuna cha ubishi. Wamehukumiwa kifo sasa hawa wajinga wanataka marekebisho gani?


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...