Mtalaam wa masuala ya Biogesi na Majiko Sanifu wa
Taasisi ya kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania (
TaTEDO) Bw.Stephen Boniface akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu ujenzi wa mtambo wenye uwezo wa kuzalisha gesi yenye mita za
ujazo 200 walioujenga katika shule ya Sekondari Manzese iliyoko
wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa
Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege akitoa ufafanusi kwa waandishi wa
habari kuhusu manufaa ya mradi wa nishati endelevu ya Biogesi
utakavyowanufaisha wanafunzi wa shule hiyo.
Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Bw. Shima
Sango kutoka Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa
Mazingira (TaTEDO) Akiwasha moja ya jiko la gesi liliojengwa katika
shule ya Sekondari Manzese.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Na.Aron Msigwa-MAELEZO
SHULE
za Sekondari kote nchini zimeshauriwa kuwekeza katika matumizi ya
Nishati endelevu ya Biogesi na majiko sanifu ili kulinda na kuhifadhi
mazingira.
Ushauri huo umetolewa na Meneja
Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam
(DAWASA) Bi.Neli Msuya mara baada ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa
kuzalisha Nishati endelevu ya Biogesi katika Shule ya Sekondari
Manzese wilayani Kinondoni, jijini Dar es salaam.
Amesema
kuwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam ( DAWASA )
ikishirikiana na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa
Mazingira (TaTEDO)na Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa UN- HABITAT
wameamua kuitumia changamoto ya uhifadhi wa Maji Taka iliyokuwa
inaikabiri shule hiyo kwa kuanzisha mradi wa kuyageuza maji taka ya vyoo
vya shule hiyo kuwa rasilimali ya kuzalisha nishati endelevu ya
Biogesi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...