Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akifanunua jambo
kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu, wakati wa maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA wakichukua
vipeperushi mbalimbali vya SSRA katika monyesho hayo.
Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka
hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi wa Zanzibar, Issa Ussi Gavu akizungumza
wakati alipotembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Juma Malik Akil.
Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimsalimu Ofisa wa SSRA, Ally Masaninga, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
(Picha zote na mpigapicha wetu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...