Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.

Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. MUNGU AMLAZE PEMA NA AWAFARIJI FAMILIA YAKE. ALIKUWA MAMA MCHAPAKAZI, SHUPAVU MWENYE UTU.

    ReplyDelete
  2. Akumpzike kwa amani.. Amen

    ReplyDelete
  3. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SISTER CELINA MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
    MATWANGA& FAMILY CANADA

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi na kuwafariji ndugu na wafanyakazi wenzake. Mama huyu alikuwa mchapakazi, muadilifu na alijawa na ubinadamu.

    Aliweza kudumu katika uwaziri kila mara baraza lilipokuwa linabadilishwa kutokana na uchapakazi na uadilifu wake na jinsi alivyojituma kuwatumikia watanzania.

    Mama Celina Kombani safari yako hapa duniani imekamilika lakini umefanikiwa na ulifanikiwa kuacha alama nzuri ya nyayo zako katika kila nafsi uliyoigusa kwa misaada yako, ucheshi wako na utumishi wako.

    Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi na awafariji wafiwa wote.

    ReplyDelete
  5. HAKIKA NI MSIBA MKUBWA KWA TAIFA. R.I.P MAMA CELINA

    ReplyDelete
  6. Poleni wafiwa Mungu awatie nguvu na kuwapatia amani wakati huu wakupoteza mpendwa wenu ambaye pia ni kati ya viongozi wa taifa hili.

    ReplyDelete
  7. Pumzika kwa amani mama Kombani, Amina.

    ReplyDelete
  8. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya sister Celina mahali pema peponi amen
    Matwanga & Family Canada

    ReplyDelete
  9. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya sister Celina mahali pema peponi amen
    Matwanga & Family Canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...