DAR ES SALAAM, Tanzania. Tarehe 21 Septemba
2015 -- Symbion Power yenye tawi lake maeneo ya Ubungo leo imetangaza kuwa
imefanikiwa katika majaribio ya kutumia gesi asilia katika mitambo yake . Gesi
inapatikana Ghuba ya Mnazi iliyo karibu na Mtwara Kusini mwa
Tanzania.
Kwa zaidi ya Mwaka mmoja sasa ; Mitambo hii yenye uwezo wa kuzalisha
kiasi cha Megawati 120 haikuweza kufanya uzalishaji wowote kutokana na ukosefu wa
gesi asilia kama chanzo cha nishati Tanzania
“Kwa mara nyingine Symbion ina uwezo wa
kufanya kazi kwa kutumia gesi asilia badala ya kutumia nishati ya mafuta ambayo
pamoja kuwa ni aghali Symbion ililizamika kuitumia kati ya mwaka 2012 na 2014”
alinena Mtendaji Mkuu Bwana Paul Hinks.
Kwa hivi sasa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) nalo litaweza kuendesha mitambo yake kadhaa ya kuzalisha umeme kwa
kutumia gesi kutoka Mtwara.
Aidha Bwana Hinks aliongeza na kusema “ Hii
ni habari njema kwa TANESCO ambayo imekuwa na wakati mgumu kifedha kutokana na
gharama kubwa inayotumia kununulia mafuta ambayo huingizwa kutoka nchi za nje.
Matokeo ya utumiaji gesi asilia katika kuzalisha umeme yatapelekea kuwepo kwa
matokeo chanya kifedha kama matokeo mtambuka ya gharama nafuu za uzalishaji
umeme”.
Mitambo ya Symbion Power iliyoko maeneo ya
Ubungo ilikuwa ni eneo kuu ambalo Rais Barack Obama alilitumia kuhutubia mnamo
Julai mwaka 2013 ambapo pamoja na mambo mengine aliainisha dhana yake ya “Power
Africa” ambayo yaweza kutafsiriwa kama Afrika yenye Umeme.Hii dhana ililenga
kwenye kuongeza upatikanaji wa umeme mara mbili katika nchi zilizo kusini mwa
Jangwa la Sahara. Kama sehemu ya “Afrika yenye Umeme” Symbion imedhamiria
kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani billion 1.8 katika sekta ya Umeme kwenye
nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kati ya Julai 2013 mpaka Julai 2018.
Kampuni
ya Symbion kwa kushirikiana na TANESCO; ziko katika harakati ya kutengeneza
mitambo mingine yenye uwezo wa kuzalisha kiwango cha Megawati 600 huko Mtwara.
Pamoja na hilo kutakuwepo nguzo za kusambaza umeme mpaka Songea Magharibi huko
Kusini mwa Tanzania na kusini mwa Msumbiji. Mara hii miradi itakapokamilika;
itaifanya Mtwara kuwa kitivo kikuu cha nishati; kwa maana hiyo itasaidia kuleta
umeme ambao unahitajika sana kwenye eneo hilo na hivi kusaidia katika
kutengeneza maelfu ya ajira nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...