Angellah Jasmine Kairuki

Tarehe 14 Septemba 2015 ulisambazwa ujumbe kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ukidai kuonyesha mawasiliano ya Makada wa Chama cha Mapinduzi nikiwamo mimi (Angellah Kairuki), Nd. January Makamba, Nd.Mwigu Nchemba na Nd.Livingstone Lusinde.  
Wakati ujumbe huo umeanza kusambazwa nilikuwa kwenye mikutano ya Kampeni ya Mgombea Mwenza wa CCM Mhe.Samia Suluhu Hassan Wilayani Nachingwea na Liwale hivyo kupelekea kuchelewa kutoa taarifa yangu hii.

Napenda kuufahamisha umma kwamba ujumbe huo uliosambazwa ni wa uwongo na hapajawahi kuwepo mawasiliano hayo popote.  Ni ujumbe uliotengenezwa kuupotosha umma kwa manufaa ya kisiasa ya walioutunga na kuusambaza.
Vilevile, napenda kuujulisha umma kwamba Mimi  binafsi situmii njia ya mawasiliano ya whatsapp na wala sijawahi kuitumia wakati wowote ule, hivyo siwezi kuwa kwenye group lolote lile  kama ujumbe uliosambazwa ulivyotaka kuuhadaa umma.
Ni vema ikaeleweka kuwa ni kosa la Jinai kujifanya wewe ni mtu fulani wakati siyo.  Hivyo naviomba vyombo vya sheria kuwasaka wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria waliotunga na kusambaza ujumbe ule kwa kutumia majina ya watu wengine.  


Natumaini TCRA nao watafuatilia chanzo cha taarifa hizo za uwongo ili washughulike na wahusika kupitia sheria ya makosa ya mtandao.

Ninawapa pole wale wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizo za uwongo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...