1. Mwezi
Machi, 2015, Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lilipitisha Sheria
ya Kuratibu Ajira za Wageni Nchini Na.1 ya Mwaka 2015 (The Non - Citizens
(Employment Regulation) Act). Sheria hii ilisainiwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei, 2015 na imetangazwa kuanza kutumika rasmi tangu tarehe 15/09/2015 kupitia Gazeti la Serikali Na. 406 la mwaka 2015.
2. Sheria hii inaanzisha Mamlaka moja ya utoaji wa
vibali vya ajira kwa wageni
na Mamlaka hiyo ni Kamishna wa Kazi.
3.
Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria hii, Wawekezaji
au Waajiri wanaokusudia kuajiri wageni nchini wanapaswa kuwasilisha maombi kwa Kamishna
wa Kazi na hati maalum ya kibali cha Ajira itatolewa kwa mgeni husika.
4.
Mgeni atakayepatiwa kibali cha ajira
atatakiwa kuwa na kibali cha Ukaazi ambacho kinatolewa na Idara ya Uhamiaji.
5.
Ada ya Vibali vya Ajira italipwa kwa
kuzingati aina ya daraja la kibali husika kama ifuatavyo;
i.
Daraja
A kwa Wawekezaji na waliojiajiri wenyewe-USD 1,000
ii.
Daraja B kwa Taaluma maalum zilizoainishwa
chini ya Sheria-USD 500
iii.
Daraja C kwa Taaluma nyinginezo-USD 1,000
iv.
Daraja D kwa walioajiriwa na Mashirika ya
Dini na ya hisani-USD 500
v.
Daraja E kwa ajili ya Wakimbizi- Bure.
Malipo au Ada ya huduma hii italipwa kupitia Akaunti inayotajwa hapa chini;
Name:
Permanent Secretary, Ministry of
Labour and Employment
A/C
No: 0250211745400
Bank: CRDB
Aidha ,Mfumo huu mpya wa
utoaji wa vibali vya Ajira kwa wageni utaanza rasmi tarehe 1/10/2015 na maombi
yawasilishwe Ofisi ya Kamishna wa
Kazi,makao Makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira,jengo la NSSF-Mwl.Nyerere Tower,Na 42,iliyopo Barabara ya Bibi
Titi Dar-es-salaam.
6. Wizara
inapenda kutoa Rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano ili kutekeleza matakwa ya
Sheria kwa ufanisi wa maendeleo ya nchi yetu.
Imetolewa
Ridhiwani M. wema
Msemaji.
Wizara
ya Kazi na Ajira.
28/09/2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...