Katika ukurasa wa mbele na wa tano wa
Gazeti la Nipashe, toleo 0578604 la tarehe 12 Septemba, 2015 kumechapishwa
taarifa kwamba “Sefue; Marufuku kutumia magari ya serikali kwenye kampeni”
Katika taarifa hiyo, imeelezwa kwamba
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema “Ni kosa kwa Wakuu wa Mikoa
na Wilaya kutumia rasilimali za serikali yakiwemo magari katika mikutano ya
kampeni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).”
Alichosema Katibu Mkuu Kiongozi ni kwamba Watumishi wa Umma
wakiwemo Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawaruhusiwi kutumia rasilimali za umma
yakiwemo magari kwenye kampeni za kisiasa isipokuwa wanapokuwa katika
utekelezaji wa majukumu yao kiserikali.
Aidha, watumishi wa Umma wanaotaka kushiriki katika katika
kampeni za kisiasa ama kugombea nafasi yoyote ya kisiasa sharti wajiudhulu
nyazifa zao za utumishi wa umma.
Kupitia taarifa hii, Watumishi wa Umma
na wa Kisiasa wanaombwa kuzipuuza taarifa hizo potofu zilizoandikwa na gazeti
la Nipashe na wanashauliwa kufuata maelekezo yaliyomo kwenye Waraka wa Mkuu wa
Utumishi wa Umma Namba 1 wa Mwaka 2015. Walaka huu unaeleza bayana utaratibu na
jinsi Watumishi wa Umma wanavyoweza kushiriki katika kugombea ama kufanya
kampeni za kisiasa na utaratibu pindi mtumishi wa umma anataka kugombea nafasi
ya kisiasa.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo
13 Septemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...