TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14.09.2015.
·
MTU MMOJA MKAZI WA MWAMBANI WILAYANI
CHUNYA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI.
·
MTU MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA
AUAWA KWA KUCHOMWA KISU SHINGONI.
·
MTOTO WA MIEZI MINNE AFARIKI DUNIA BAADA
YA NYUMBA ALIMOKUWA AMELALA KUUNGUA MOTO.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA MKAZI WA MWAMBANI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NTIGA LUFWEGA (35) AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ZA BUNDUKI AINA YA GOBOLE UBAVU WA
KUSHOTO NA MTU ALIYEMFUATA NYUMBANI KWAKE ILI AKAMUUZIE NG’OMBE ENEO LA
MAKAMBINI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.09.2015
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MWAMBANI-CHINI, KIJIJI NA KATA YA MWAMBANI, TARAFA YA
KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA
KUWA, MAREHEMU ALIKUWA NA PIKIPIKI YAKE YENYE NAMBA ZA USAJILI T.587 CWO AINA YA FEKON HUKU AKIWA
AMEMPAKIZA MTU HUYO NA NJIANI ALIMPIGA RISASI KISHA KUONDOKA NA PIKIPIKI HIYO
PAMOJA NA SIMU YA MAREHEMU AINA YA ITEL.
PIKIPIKI
IMEPATIKANA KATIKA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI IKIWA IMETELEKEZWA MARA BAADA YA
KUISHIWA MAFUTA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI EDWARD (26) AFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA BAADA YA KUCHOMWA KISU SHINGONI NA MTU ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.09.2015
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA WAKATI
MAREHEMU AKIWA NYUMBANI KWAKE HUKO ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO
BADO KINACHUNGUZWA, UPELELEZI UNAEDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATUHUMIWA WA MATUKIO HAYA YA MAUAJI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE HATUA ZAIDI ZA KISHERIA DHIDI YAO.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MTOTO
WA MIEZI MINNE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZABETH
MWALUPEMBE MKAZI WA MBANGA WILAYANI CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA NYUMBA
ALIMOKUWA AMELALA KUUNGUA MOTO NA KUTEKETEZA MALI ZILIZOKUWEMO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.09.2015
MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MBANGA, KIJIJI CHA MAPOGOLO, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA
KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
NYUMBA
HIYO AMBAYO NI MALI YA PETER RICHARD MWALUPEMBE (30) MKAZI WA
MBANGA YENYE CHUMBA NA SEBULE ILIYOEZEKWA KWA BATI ILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MWENYE NYUMBA KUMIMINA MAFUTA AINA
YA PETROLI KWENYE DUMU HUKU MSHUMAA UKIWA PEMBENI UNAWAKA HIVYO MOTO KULIPUKA WAKATI
MAREHEMU AKIWA CHUMBANI AMELALA.
AIDHA
KATIKA TUKIO HILO PETER RICHARD
MWALUPEMBE AMEJERUHIWA KWA KUUNGUA MOTO MWILI MZIMA NA HALI YAKE NI MBAYA.
MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA. THAMANI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...