
Eng. Kelvin Komba akitoa mada kuhusu hali ya utafutaji na muendelezo wa uzalishaji katika shughuli za gesi asilia na mafuta. Baadhi ya mada zilizowasilishwa ni kuhusu sera, sheria na mipango ya serikali katika sekta ya gesi asilia na mafuta; na fursa za ushirikishwaji wa watanzania katika mnyororo wa shughuli za gesi asilia na mafuta.
Wadau wa sekta ya gesi asilia na mafuta kutoka taasisi mbali mbali wakifuatilia warsha hiyo. Mada zingine
zilizowasilishwa ni madhara ya kijamii na kimazingira kutokana na uchimbaji wa nishati hizo; pamoja na wajibu wa wadau wa serikali za mitaa katika kuendeleza sekta hiyo.
Wadau wa sekta ya mafuta na gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha warsha ya siku moja iliyokuwa inahusu nafasi ya wadau kutoka ngazi za mkoa, wilaya na halmashauri katika usimamizi wa rasilimali za mafuta na gesi asilia iliyofanyika mkoani Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...