
Mwakilishi kutoka shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada
ya kukagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandi katika uwanja wa mpira wa
Kaitaba Amewaomba mafundi kuongeza kasi ili ukamilike kwa muda
uliopangwa. Mwakilishi huyo wa FIFA Mhandisi Kelvin Macklain, alitua
Bukoba wiki iliyopita na kukagua hatua kwa hatua uwanja huo na alifika
hapo kukagua hatua za mwisho kabla ya nyansi husika kuanza kutandazwa,
ambazo tayari zipo katika uwanja huo.
Hata hivyo Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba
Malick Tibabimale, alisema kuwa sehemu ya kati ya uwanja itakamilika
ndani ya mwezi mmoja, na timu ya Kagera sugar itaanza kuutumia uwanja
huo baada ya mechi zake nne za mzunguko wa kwanza.
Timu ya Kagera Sugar kwa sasa itaendelea kutumia Uwanja wa Musoma kama uwanja wake wa nyumbani katika Ligi kuu ya vodacom iliyoanza kutimua vumbi jumamosi septemba 12, 2015.
![]() |
Nyasi bandia zikiwa zimewekwa pembeni ya Uwanja tayari kwa kutandikwa katika Uwanja huo
|
Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja huo Pierre De Groote baada ya kuukagua Uwanja huo alisema watamaliza kazi yote mwezi Desemba mwaka huu 2015.
Mhandisi Kelvin Macklain Mwakilishi kutoka FIFA akifanya vipimo katika Uwanja wa Kaitaba unaoendelea kujengwa mpaka sasa. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com

Sehemu ya katikati ya Uwanja wa Kaitaba ambayo itakamilika mwezi huu wa tisa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...