Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa, Sifuni Mchome akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba wa mkopo kati ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA, Joel Laurent na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TIE,Dk.Paul Mushi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome akisaini makubaliano ya mkataba wa mkopo kati ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA,Joel Laurent na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TIE,Dk.Paul Mushi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa TEA na TIE mara baada ya kumalizika makubaliano kati ya taasisi hizo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeingia makubaliano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) ya mkopo wa sh.Bilioni Tatu kwa ajili ya kuiwezesha TIE kufanya utafiti wa kubaini mahitaji ya mabaoresho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu.
Katika utafiti huo TIE itaandaa mitaala na mihtasari ya masomo ya shule ya msingi, kuandika vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la Sita ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuingia makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA,Joel Laurent mkataba wa mkopo huo ni nafuu ambao unatakiwa kulipwa katika kipindi cha miaka sita.
Amesema TEA itaendelea kushirikiana na TIE kwa kuzingatia sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 na TIE kuridhia mkopo maombo ya mkopo ili kuhakikisha uwepo mihtasari ,Mitaala na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita vinavyoendana na mahitaji.
Kwa upande Mkurugenzi Mkuu wa TIE, Dk.Paul Mushi amesema matokeo tarajiwa kutokana na mkopo huo ni pamoja na uwepo wa mitaala inayoendana nan a wakati na inayokidhi mahitaji ya sekta shirikishi ,uwepo wa mihutasari ya masomo itakayosambazwa katika kila shule kama ilivyoainishwa katika mitaala na uwepo wa vitabu vya kiada kulingana na mitaala ili kuepusha kuwa na vitabu vinavyotaofautiana.
Aidha amesema ufadhili unalenga kuiongezea TIE kuelekeza majukumu yake kwa njia yenye tija na kuongeza mapato ya taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...