Fuso
ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar,
Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi-
Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya na Songea
ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
Na Mwandishi Wetu,
MTANDAO wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na
kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli
ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba
3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika
katika usafirishaji wa mizigo.
Usafirishaji
nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji
ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na
maji na anga. Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za
Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa
zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”
Wakati
ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa
njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa
usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake,
kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa
cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...