‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au yanayodunda sana. 

Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. 

Ingawa, kama mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au yasiyoimara.
Kuna aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia, Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation.
Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.

Kusoma zaidi bofya HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...