
LISSA ALIMFAHAMISHA MHARIRI WAKE JUU YA TAARIFA HIZO, AMBAPO MHARIRI
ALIMTAKA KUFUATILIA TUKIO HILO.
MWANDISHI HUYO ALIONDOKA OFISINI SAA 2:50 ASUBUHI MPAKA KINONDONI
ENEO AMBAKO WAANDAMANAJI WALIKUWA
WAMEPANGA KUANZIA MAANDAMANO YAO.
WAANDAMANAJI WALICHELEWA KUFIKA ENEO TAJWA NA ILIPOTIMU SAA 5.00
NDIPO WALIFIKA WAKIWA KWENYE BASI NA KUSHUKA KUANZA MAANDALIZI YA
MAANDAMANO HUSIKA.
WAANDAMANIJI HAO WALIANZA MAANDAAMO MUDA MFUPI BAADAYE KUELEKEA
OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CHADEMA ZILIZOPO MTAA WA UFIPA, KINONDONI.
HUKU WAKIWA NA MABANGO YALIYOKUWA NA UJUMBE TOFAUTI AMBAPO MWINGI
ULIKUWA UKIKEMEA KITENDO CHA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA, EDWARD LOWASSA, KUTUMIA
UDINI KUOMBA KURA KANISANI. ITAKUMBUKWA KWAMBA LOWASSA ALIOMBA KURA HIVI
KARIBUNI ALIPOKUWA MJINI TABORA, AMBAPO ALIFANYA HIVYO KATIKA KANISA LA KILUTHERI.
BAADA YA KUNDI HILO LA WAANDAMANAJI KUFIKA, LILIKWENDA MOJA KWA MOJA
HADI KATIKA MLANGO WA KUINGIA KWENYE OFISI ZA CHAMA HICHO, AMBAPO MWANDISHI
WETU ALIANZA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE AKIWA NA WAANDISHI WENGINE.
HATA HIVYO KATIKA HALI YA KUSHANGAZA LISSA PAMOJA NA WAANDISHI WENZAKE
WA HABARI, WALIKAMATWA NA WALINZI WA CHAMA HICHO, AMBAPO WENZAKE WALIACHIWA
BAADA YA KUJITAMBULISHA KUWA WANATOKA VYOMBO VYA HABARI.
LAKINI CHA KUSHANGAZA LISSA ALIPOJITAMBUSHA KUWA ANATOKA GAZETI LA UHURU
NDIPO WALIPOSEMA KWAMBA ‘HUYU NDIYE TULIYEKUWA TUNAMTAFUTA’ NA KUANZA KUMPIGA KWA
NGUMI MAGONGO NA VYUMA NA KUMSABABISHIA MAJERAHA NA KUHARIBU KAMERA, HUKU
WAKIMPORA SIMU YAKE YA MKONONI NA ‘WALLET’ ILIYOKUWA NA JUMLA YA SH. 80,000.
AIDHA ALIPOKUWA AKIPIGWA WAHUSIKA WALISIKIKA WAKISEMA TUWASUBIRI
WAKUBWA NA MUDA MFUPI BAADAYE ALIINGIA MSEMAJI WA CHAMA HICHO, BONIFASCE
MAKENE, DIWANI WA UBUNGO CHADEMA, AMBAYE
PIA ANATUHUMIWA KUMSHAMBULIA MLINZI WA DK.
WILLIBROD SLAA, MUDA HUO HUO PIA
ALIPITA MHE. JOHN MNYIKA ALIYEKUWA NA
KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI.
KWA MUJIBU WA MWANDISHI LISSA ALIYEELEKEZA NA KUMUINGIZA KWENYE CHUMBA
CHA MATESO NI DIWANI HUYO WA UBUNGO AKIWA PAMOJA NA WALINZI WENGINE AMBAO
WALIKUWA WAKIMPIGA.
AKIWA KATIKA CHUMBA HICHO ALIENDELEA KUPIGWA NA BAADAYE ALIPEWA KADI
ZA CHADEMA NA KUANZA KUSHURUTISHWA KUSHIKA HIZO KADI NA ATAMKE MBELE YA KAMERA
YA VIDEO ILIYOKUWA IKIMREKODI KWAMBA YEYE AMETUMWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA
MAPINDUZI (CCM), ABDULRAHMAN KINANA NA VIONGOZI WA CCM KUANDAA MAANDAMANO HAYO,
AMBAPO PAMOJA NA KUSHURUTISHWA HUKO ALIKATAA NA KUSHIKILIA MSIMAMO WAKE KWAMBA
ALIKUWA AKITETEJELEZA MAJUKUMU YAKE YA UANDISHI WA HABARI NA SI VINGINEVYO.
WAKIWA WANAAENDELEA KUMSHURUTISHA GHAFLA WALIINGIA POLISI NA WATEKAJI
WALISTUKA NA KUMWELEZA ASISEME KWAMBA ALIKAMATWA NA YUKO NDANI, HIVYO WALIMTOA
NA KUTOKA NAYE NJE PAMOJA NA WATU WENGINE HUKU AKILINDWA NA WALINZI WA CHADEMA.
POLISI WALIPOFIKA NA KUOMBA KUFANYA UPEKUZI KUTOKANA NA TAARIFA ZA KUWEPO
MWANDISHI WA UHURU, ANAYESHIKILIWA NDANI YA OFISI, WALIRUHUSIWA KUFANYA HIVYO
HUKU LISA AKIWA NJE NA WALINZI WA CHADEMA WALIOMTAKA KUTOJITAMBULISHA AU KUSEMA
CHOCHOTE WAKATI POLISI WAKIWEPO ENEO HILO.
BAADA YA POLISI KUONDOKA WALISIKIA WAKISEMA KWAMBA ‘DILI’ YETU
HAIJAFANIKIWA NA KUINGIA NAYE NDANI TENA NA KUMWELEZA MNYIKA ALIYEKUWA
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWAMBA WAMEMKAMATA MWANDISHI WA UHURU AMBAYE
NI MUANDAAJI WA MAANDANAMO HAYO.

PAMOJA NA VITISHO HIVYO, LISSA ALIKATAA NA KUSHIKILIA MSIMANO WAKE
KWAMBA ALIFIKA ENEO HILO KUFANYA KAZI YAKE YA UANDISHI WA HABARI NA SI VINGINEVYO.
BAADHI YA WAANDISDHI WALISIKIKA WAKISEMA KWANINI MWENZAO ALIKUWA AKISHURUTISHWA
KUSEMA MANENO HAYO.
WALINZI HAO WAONEKANA KUKIRI KWAMBA ZOEZI LAO LIMESHINDIKANA NA WENGINE
WALITAKA APIGE NA HADI KUFA ILI KUPOTEZA USHAHIDI, LAKINI WENGINE WALIGOMA
WAKISEMA HAPO NI MAKAO MAKUU YA CHAMA.
BAADA YA KUTOFAUTIANA WENYEWE KWA WENYWE WALIMRUHUSU LISSA AONDOKE NA
NDIPO ALIPOONDOKA NA GARI LILILOKUWA NA WAANDISHI WA HABARI WA AZAM MOJA KWA
MOJA KWENDA KITUO CHA POLISI, OYSTERBAY AMBAKO ALITOA MAELEZO YAKE.
TUNASIKITIKA KWAMBA CHADEMA WAMEAMUA KUFANYA SIASA CHAFU
ZINAZOTUHUSISHA KATIKA HARAKATI ZAO AMBAZO ZIMESHINDWA KUFANIKISHA KUWASHAWISHI
WATANZANIA ILI WAWACHAGUE.
AIDHA, TUNALAANI VIKALI KITENDO HICHO KILICHOFANYWA NA KUNDI LA
MAOFISA NA WALINZI WA CHAMA HICHO, KUINGILIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.
CHADEMA WAMEFANYA UNYAMA HUO DHIDI YA MWANDISHI WETU, LAKINI CHAMA CHA MAPINDUZI
HAKIJAWAHI KUFANYA HIVYO. HIVYO TUKIO HILI LIMEONYESHA PICHA HALISI CHA CHAMA
HICHO AMBACHO KINALILIA KUWAONGOZA WATANZANIA.
WAKATI TUNALAANI UNYAMA HUO, TUNAAMINI VYOMBO VYA HABARI VITAKEMEA TUKIO
HILI, LAKINI PIA TUNAAMINI HATUA STAHIKI ZA VYOMBO VYA DOLA IKIWEMO POLISI
VITACHUKUA HATUA DHIDI YA WALIOHUSIKA NA UNYAMA HUO.
DAIMA CCM IMEKUWA IKIENDESHA KAMPENI ZA KISTAARABU KATIKA KIPINDI HIKI
CHA UCHAGUZI MKUU TOFAUTI NA CHADEMA. UONGOZI WA UPL UNATOA POLE KWA LISSA NA
KUMTAKIA MATIBABU MEMA.
RAMADHANI MKOMA,
KAIMU MHARIRI MTENDAJI,
UHURU PUBLICATIONS LIMITED
ReplyDeleteHata watu si wazuri ... mimi nimeshambuliwa kama mara mbili na nimetoa taarifa kwa viongozi wa CCM lakini bado nafuatilia
Hakuna sababu ya kupigana ni kipindi cha wanasiasa kutafuta kura sasa ushabiki wa kupigana na kupiga wasiokuwa wanasiasa unatoka wapi?????
ReplyDeleteHili tukio limetokea lini???
ReplyDeleteNINYI NI WAZUSHI NA WACHAFUZI WA AMANI. HAYO MAANDAMANO NI CCM MLIYAANDAA KAMA AMBAVYO MMEENDELEA KUFANYA KWA KUWAANDAA VIJANA NAKUWAPA FULANA ZENYE UJUMBE KUONYESHA NI CHADEMA WAKATI SIO. HATA RWANDA NI SERIKALI NA CHAMA KILICHOKUWA MADARAKANI NDIO WALIKUWA CHANZO CHA MAUAJI YA HALAIKI HAPO 1994, SABABU KUBWA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA. "CCM HAIWEZI ZUIA MABADILIKO AMBAYO WANANCHI WANAYATAKA, TUMEWACHOKA NA UCHONGANISHI WENU. KULE MKOA WA MARANI JUZI TU CCM HAO HAO WAMEUA MTU MFUASI WA CHADEMA. MBONA HAMUYAANDIKI?"
ReplyDeleteWewe mdau wa nne acha propaganda zisizokuwepo na jazba zisizokuwa na tija.
ReplyDeleteUtasubiri sana mabadiliko ccm ni ileileukitaka kchukue uraia wa china
ReplyDelete