Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WANAFUNZI waliosoma  Shule ya Forodhani na Sasa St.Joseph Cathedral  wameanzisha  umoja wa shule hiyo kwa ajili ya kusaidia elimu pamoja na masuala ya kijamii.

Wakizungumza nyakati tofauti wanafunzi waliosoma hapo wamewataka wanafunzi kufuata nyayo zao kutokana na shule hiyo kuwa na historia nzuri ambayo hadi sasa haijaweza kufutika.

Wamesema kuwa umoja huo utakuwa imara katika kusaidia shule hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo na kusaidia jamii kutokana na malezi walioyapata katika shule hiyo tangu Ukoloni.

Akizungumza katika uzinduzi huo mwanafunzi aliosoma shule hiyo,Mariam Zialor, amesema umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent school  iliodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969, na Forodhani Sekondari  ilokuwapo 1970 hadi 2008 ( ilitaifishwa na serikali) na baada ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurushwa kwa kanisa la katoliki)  hadi leo inatambulika   St. Joseph & Forodhani  ALUMNI .
Miriamme amesema katika shule hiyo  kuna wanafunzi waliosoma shule hiyo, wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka  Canada, Australia, New Zealand Uingereza na Seychelles wameungana kuhudhuria mkutano huu wa kishitoria wa kuanzisha umoja wa ALUMNI.

Amesema baadhi ya wanaWengine hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30.  Wanarudi kuona shule iliowalea.

Aidha amesema katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles  ambaye alisoma hapo na kumaliza kidato cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo  kuendelea na masomo ya juu.

Kwa upende wa Mbunge wa Viti Maalumu ,mwanafunzi wa shule hiyo zamani Ashymaa Kwegyry ametaka wanafunzi kuwa wadhubutu na kuweza kufanikisha ndoto zao.

Amesema amesoma shule kutokana na kuwa na ulemavu lakini walimu walimfundisha na kuamini kuwa na anaweza kufanya kitu kama binadam wengine.
Mwanafunzi wa Zamani wa Forodhan,Mariam Zialor akizungumza wakati wa uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma shule ambayo kwa sasa ni St.Joseph Cathedral leo jijini Dar es Saalaam.
Mwananfunzi wa zamani wa shule ya Sekondari ya St.Joseph hivi sasa, Ashymaa Kwegyry akizungumza katika uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph walioshiriki katika uzinduzi wa umoja wa wanafuzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph zamani wakiwa wameshuriki katika uzinduzi wa wanafunzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wakitumbuiza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai mara baada ya kucheza ngoma inayowakilisha kabila la wamasai katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo. 
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph 
 Picha ya pamoja ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph mara baada ya kumalizika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Big up Michuzi. Good old memories... way back those days from nursery school to secondary school.!

    ReplyDelete
  2. Hata mimi ni old girl wa shule hii, nilishajiandikisha, tusaidie kuboresha shule tulizotoka enzi hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...