Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau
wote
wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania
kwa
mwaka 2016 kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa
hadi
tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi hayo.
Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa
na
mashindano katika ngazi ya wilaya wala Kanda.
Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na:
1) Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka
husika ya Serikali.
2) Uwe na mtaji wa kutosha.
3) Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika
ufanisi mkubwa.
4) Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa
za utamaduni nchini.
Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania
atapaswa
kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla
hajapewa
kibali cha kuandaa shindano.
Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na
Temeke
zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa
Elimu
ya Juu.
Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja.
Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania
baada ya
maombi kukubaliwa na kupitishwa.
Maombi yatumwe kwa barue pepe misstanzania2015@yahoo.com
Damn all these girls would have been miss world what a waste
ReplyDelete