KUSOMA ZAIDI
links goes to
sheriayakub.blogspot.com
Na Bashir
Yakub.
KISHERIA haizuiwi kuweka
rehani nyumba ya
makazi kwa ajili
ya kupata mkopo
kutoka taasisi yoyote
ya fedha. Jambo la msingi sana
ni kuwa watoa
mkopo wajiridhishe na
umiliki wa nyumba
hiyo hasa kwa
kuangalia ikiwa ni mali
ya familia au
hapana ili wachukue hadhari za
kisheria.
Nyumba ya makazi
ni ipi. Nyumba ya makazi ni
ile nyumba ambayo
inatumiwa na binadamu
kuishi lakini zaidi
wanaoishi mle ndani
iwe ni familia
ya mchukua mkopo. Yawezekana
nyumba ikawa ni ya makazi
kwa watu
wengine lakini ni ya biashara
kwa mchukua mkopo. Kwa
mfano nyumba za
kupanga ambapo mwenye
nayo anaishi kwingine
na nyumba iko kwingine ikiwa na watu wengine.
Nyumba ya
namna hii haitaingia
kwenye nyumba ya
makazi kwa tafsiri
hii. Hata hivyo
haitarajiwi mchukua mkopo
kuhamia kwenye nyumba
ambayo sio ya makazi kwa
makusudi na kuifanya ya
makazi akilenga kuhadaa
ili kupata upendeleo
wa mahakama. Akifanya
hili atakuwa amedanganya
na ni kosa
kama tutakavyoona.
1.MAKOSA YA
KISHERIA KWA MKOPAJI.
( a ) Sheria ya masuala ya
rehani ya 2008
inamtaka mkopaji kutofanya
udanganyifu wa aina
yoyote kwa taasisi inayotarajia kumpa mkopo. Moja ya
udanganyifu ni kama
ilivyoelezwa hapo juu
lakini pia upo
udanganyifu mwingine mwingi
ambao hufanywa na wakopaji. Kwa
mfano kuweka rehani
nyumba moja kwa
taasisi tofauti, kudanganya
nyumba sio ya
familia wakati ni
ya familia na udanganyifu mwingine
mwingi ambao hulenga
kumnufaisha mkopaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...