Meneja wa Program wa Restless Development,Oscar Kimaro akizungumza na vijana (Hawapo Pichani )kutoka asasi mbalimbali kuelelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyofanyika katika Makao Makuu Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Asasi ya Hope Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015 Tanzania,Tumaniel Mangi akizungumza na vijana (hawapo pichani) juu ya kuwa mabalozi wa malengo 17 ya SDGs katika mkutano uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakiwasha mishumaa kuashirishia kuonyesha njia ya utekelezaji wa Malengo 17 ya SDGs, katika mkutano uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka.
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
LEO Septemba 25 hadi 27, wakuu wa
nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana jijini New York, Marekani kwa ajenda ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanayoanzia
2016 -2030.
Katika mkutano huo, nchi wanachama watapitisha ajenda za (SDGs) zenye Malengo 17 ya ambayo ni kukomesha umaskini,
kuhamasisha usawa na kupinga uonevu, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,Afya
Bora,Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Ujengaji wa Uchumi na Ajira zenye
staha,Uboroshaji wa Majiji na Mitaa,Mahusiano ya Kimataifa ,Utawala wa Sheria
na Haki na mengine mengi kufikia mwaka 2030.
Malengo hayo ni dira ya Ulimwengu na kufika
mwisho kwa malengo Nane ya Millenia katika kupambana na umaskini ambayo
ulimwengu uliazimia kutafikia kwa mwaka 2015.
Meneja wa Program wa Taasisi ya
Restless Develoment,Oscar Kimaro amesema malengo ya SDGs
ni vijana na wanawajibu kuwa mabalozi
kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa
kutokana na kuwepo kwa changamoto zinazoikabili kama nchi.
Kimaro akizungumza katika mkutano wa
vijana katika kuelekea malengo ya SDGs amesema vijana wanakabiliwa na
changamoto kubwa likiwemo suala upatikanaji wa elimu.
Katika Mkutano wa vijana waliwasha
mishumaa kuonyesha njia kwa malengo hayo na viongozi kuweza kuridhia kama nchi haiwezi kujitenga
katika dira hizo ambayo dunia inaatamia.
Mkurugenzi wa Asasi ya Hope
Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015
Tanzania,Tumaniel Mangi amesema malengo
ya SDGs yana ushirikishwaji hivyo inahitaji utashi wa kisiasa kusukuma malengo
hayo.
Mangi amesema vijana ni sehemu ya
kuleta msukumo chanya kwa kuyasemea masuala ya SDGs kuanzia ngazi ya chini kutokana na ushirikishwaji uliopo wa malengo
hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...