KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia
kufanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
imetangaza kiingilio kwa VIP ni shilingi 5000 kwa watakaohudhuria katika
tamasha hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions, Alex Msama viti vya kawaida watalipa shilingi 3000.
Msama alisema watoto watachangia shilingi 1000 ambako alitoa
wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya
amani katika nchi yetu.
Msama alisema katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali
watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagiza
maombi hayo kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
Aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni
ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya
Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.
“Watanzania tunatakiwa tujitokeze
kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na
tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za
Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.
Alisema baada ya kumalizika
jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba
8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13
(Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga)
na Oktoba 18 (Mwanza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...