Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VIONGOZI wa nchi wametakiwa kushiriki katika mkutano wa umoja wa Mataifa wa kujadili malengo 17 ya maendeleo endelevu utaofanyika Septemba 25 mwaka huu nchini Marekani.

Akizungumza na waandishi  habari leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Mabadilliko ya Tabia nchi (CAN), Sixberty Mwanga ,amesema kuwa mkutano huo ni muhimu katika kuweza kutekeleza eneo la mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kadri ya siku zinavyoongezeka hali ya ukame inazidi kuongezeka.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa mabadiliko ya tabia ya nchi  nchi inatakiwa kutumia dola za Kimarekai bilioni 1000  kwa mwaka  na hiyo inatokana na mabadiliko katika ukame na utowekaji wa maji  pamoja na uharibifu wa miundombinu  inayotokana mafuriko.

Aidha amesema mkutano wa maendeleo  endelevu unahitaji  utashi wa kisiasa wa kuweza kufanikisha malengo ya hayo ikiwemo suala la mabadiliko ya tabianchi  ambalo linahitaji rasilimali za kutosha.

Mwanga amesema  mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa na vitu vingi ambavyo vinatkiwa kuepukwa kwa kuweza kutumia vitu asili kama matumizi ya nishati mbadala.

“Malengo 17 ya Maenndeleo Endelevu utekelezwaji wake itawezekana kama dhana ya mabadiliko ya tabianchi yatazingatiwa kwa vitendo”amesema Mwanga.

Aliongeza kuwa kuongezeka kwa njaa ikwa ni lengo la maendeleo endelevu ambayo inatokana ukame ambao umebasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa maendeleo endelevu ya mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika nchini Marekani Septemba 25 mwaka huu. 
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga akizungumza na waandishi wa habari npamoja na wadau wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa jijini Dar es Salaam leo, kulia ni  Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere
 Kulia ni Afisa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Onditi Msololo na Mhasibu wa Mradi wa mtandao wa mabadiliko ya hali ya hewa, Erick Makere wakimsikiliza Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko hali ya hewa ,Sixbart Mwanga leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...