Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari juu ya matumizi ya dawa katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yawe na uwiano sawa na kuwa na kiwango kinachokubalika Kimataifa. Amesema mamlaka husika inapaswa kusimamia na wataalam wa dawa ili kuendana na soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi namna wananchi watapata dawa zilizo bora na salama zaidi kwa kutumia vigezo vya kikamataifa kwa kuwa kuzingatia masharti yanayotolewa na Shirika la Afya Duniani. Amesema Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa uhamasishaji huu kwa wadau wazalishaji na wasambazaji wa dawa na wote wanaojihusisha na biashara ya dawa na kwamba hii ni jumuiya ya kwanza katika bara la Afrika kutekeleza mpango wa kuwa na mifumo ya aina moja ya uthibiti wa dawa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sehemu ya wadau wa dawa walio hudhulia kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo wakifurahia jambo baada ya kikao hicho (Picha na Emmanuel Mssaka)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...