Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo katika maduka ya Shoppers plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kushoto ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka hilo Bw.Argylle Tsvakai na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
 Mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania Bw.Argylle Tsvakai (kulia) akiangalia moja ya simu zinazouzwa kwa bei nafuu katika duka hilo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi na Afisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto). Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
 Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimfanyia mahojiano Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wao walioshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo leo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...