Meneja Mwandamizi wa Benki Upande
wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria (kushoto) akimkabidhi Katibu mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawii wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando (kulia) tuzo ya mfano wa hundi ya
shilingi milioni 10 kwa niaba ya wanafunzi nane na walimu wanne bora wa masomo
ya biolojia na kemia.
Meneja Mwandamizi wa Benki Upande
wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa
wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne
na sita katika hafla ya utoaji tuzo.
Afisa Mauzo wa NMB, Joseph
Mang’ongo akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Aya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Donald Mmbando kadi ya akaunti ya chapchap wakati wa maonesho yaliyokwepo
katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia
na kemia kitaifa.
Wanafunzi na walimu bora wa masomo
ya biolojia na kemia kitaifa katika hafla ya kuwakabidhi tuzo kwa kuibuka
vinara iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya meza kuu, Uongozi wa Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali na wanafunzi na walimu katika hafla ya utoaji tuzo kwa
wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne
na sita jijini Dar es Salaam.
----------------------------------
Katika kutambua jitihada za wanafunzi na walimu
nchini, Benki ya NMB imewatunukia tuzo wanafunzi nane waliofanya vizuri zaidi
kwenye masomo ya biolojia na kemia kitaifa na walimu wanne waliowawezesha
wanafunzi hao kuwa vinara katika masomo hayo tuzo ya jumla ya shilingi milioni
10 mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Kila mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi kwenye masomo
hayo mawili amejishindia jumla ya shilingi milioni 1 na kila mwalimu shilingi
laki 5.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Upande wa Taasisi -
Noelina Kivaria alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando ambaye
alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Bi.Kivaria aliwapongeza wanafunzi hao kwa jitihada
zao shuleni na kuwaasa wanafunzi wengine wachukulie hiyo kuwa ni sehemu ya
changamoto kwao hivyo wakaze kamba ili nao waweze kuwa vinara katika masomo
yao.
Benki ya NMB imekuwa ikiipa sekta ya elimu nchini kipaumbele
cha hali ya juu kwa kushirikiana na shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es
Salaam ikitoa misaada mbalimbali kama madawati.
Wanafunzi
waliotunukiwa tuzo hizo ni:
1. Samwel
Felician-Nyamanoro Secondary School
2. Jenipher
Naali-St. Francis Secondary School
3. Joshua
Zumba-Uwata Secondary School
4. Monica
Mtei-Marian Girls Secondary School
5. Felister
Silvester-Ifunda Tech. School
6. Mariam
Mzingi-Feza Girls Secondary School
7. Elisha
Mmari-St. Mary Goreti Secondary School
8. Innocent
Yusufu-Feza Boys Secondary School
Walimu
waliotunukiwa tuzo ni:
1. Halima
Tajiri-Feza Girls Secondary School
2. Rogasian
Fisso-Uwata Secondary School
3. Grolius
Rwabutomize-St. Mary Goreti Secondary School
4. Jane
Lalika-Marian Girls Secondary School
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...