Na Woinde Shizza,Arusha
Wanafunzi wametakiwa kuwekeza katika elimu, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha ya sasa na ya baadaye ikiwemo kufanya kazi kwa vitendo ,na mashiko vitavyowasaidia kwenye maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kulijenga taifa lao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum,Mr Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni,wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Katika mahafali hayo wanafunzi wanane walihitimu mafunzo ya ukatibu muhtasi ualimu wa shule za awali (chekechea) ambapo wote watapata ajira katika shule na vyuo mbalimbali vilivyopo ndani na nje ya nchi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi mtendaji wa chuo cha Full Bright College Mr.Julius Matiko amewaasa wahitimu wajiongeze na wazidisshe bidii katika elimukwani chuo hicho kina vifaa vya kutosha vikiwemo vifaa vya kompyuta,uhazini ambavyo vipo na hotel management .Chuo hicho kimesajiliwa na VETA ambapo pia wanatoa mafunzo ya NABE(National Business Examination)
Mku wa chuo hicho Rose Mapunda amewasihi na kuwashauri wazazi wawalete wanafunzi chuoni hapo wajipatie elimu na maarifa ya kutosha zikiwemo stadi za kazi mbalimbali iliwatakapotoka chuoni hapo waweze kupata ajira na kujiajiri.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha Full Bright Mr .Julius Matiko ameiomba serikali itoe ruzuku kwa vyuo binafsi ikiwezekana itoe usafiri pamoja na kutoa vifafa mbalimbali vya kujifunzia na kujisomea katika chuo hicho.
Akitaja Changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa ardhi ,wa kujenga nyumba za walimu nyumba za kulala wanafunzi, maktaba za kujifunzia na viwanja vya michezo kwa wanafunzi na wahitimu wa chuo hicho cha Full Bright
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...