MWAKA 2004, John Kitime ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (Tanzania Musicians Network-TAMUNET) alihudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Muziki Duniani –International Federation of Musician (FIM). Katika mkutano huo moja ya maazimio ya mkutano ule ilikuwa kila nchi ihakikishe inaanzisha utaratibu wa Bima ya Afya kwa wanamuziki wake. 

Mara baada ya kurudi Tanzania, kwa kushirikiana na viongozi wengine wa TAMUNET, Kitime alianza kufuatilia uwezekano wa kupata huduma ya Bima hiyo kwa wanamuziki.

 Kwa bahati mbaya hakukuwa na njia yenye gharama nafuu ya malipo ya Bima hiyo ambayo mwanamuziki wa kawaida angeweza kuyamudu. 

Kulikuwepo na kampuni ambayo iliweza kutoa huduma hiyo kwa gharama ya dola 300 kwa mwaka kwa mwanamuziki mmoja,kampuni nyingine za bima zilizotembelewa hazikuonyesha ushirikiano katika jambo hilo. 

TAMUNET iliwasiliana pia na mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa katika kipindi hicho mfuko ulikuwa hauna mamlaka ya kuhudumia watu waliokuwa nje ya ajira ya serikali na mashirika ya umma. 


Louiza Nyoni akionyesha kadi yake mpya ya Bima ya Afya
Ushirikiano wa Mfuko wa Bima ya Afya na TAMUNET unaweka uwezekano wa mwanamuziki kuanza kuchanga hata fedha kidogokidogo ili kuweza kufikisha kiasi kinachotakiwa.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...