Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Amani, Alex Msama.
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Amani, imesema inapata wakati
mgumu kuhusiana na idadi ya waimbaji ambao wanaomba kushiriki tamasha hilo litakalofanyika
Oktoba 4, mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama amesema wiki hii kuwa idadi
ya wanaoomba washiriki tamasha hilo imekuwa kubwa kuliko kawaida, ambapo hadi juzi walikuwa waombaji wamefikia 74.
“Tunapata maombi mengi, tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kujipanga
ili kuweza kila mmoja ashiriki, lakini tuna vigezo ambavyo tunaviangalia
kwanza,” alisema.
Msama amesema
tamasha hilo pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa
za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Afrika Kusini na Zambia.
"Waimbaji
wengi maarufu wa muziki wa injili watakuwepo, tumejipanga vizuri kuhakiksha
tamasha hili linakuwa gumzo kila mahali.
"Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi
kwani watashiba kiroho kwa vile kutakuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya
kiroho," alisema Msama.
Msama amesema lengo la kuwajumuisha wasanii hao
ni kutaka kulifanya tamasha hilo lenye lengo la kuombea amani liwe bora na
lenye tija kwa Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...