Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Amani linatarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali wamepania kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki watakaojitokeza.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa wiki hii na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa wasanii hao wamesema kuna mambo mazuri watayafanya siku hiyo.

Baadhi ya wasanii waliotajwa kwamba watatumbuiza siku hiyo ni Sarah K, John Lissu, Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Boniface Mwaitege.

Taarifa hiyo inawakariri wasanii mbalimbali wakizungumzia tamasha hilo, huku wakitamba kwamba mambo yatakuwa mazuri.

“Nimedhamiria kuwapa mambo mazuri mashabiki wangu, najua watafurahi sana, watakaokuja hawatajuta,” ni kauli ya Rose Muhando.

Naye msanii Upendo Nkone, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwa wana imani kubwa litakuwa tamasha zuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...