Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda gari la Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jana jijini Dar es Salaam katika ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi wa DART kabla ya kuanza kutumika .
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Wanaohujumu miundo mbinu walipe, na hizo pesa ziwekwe kwenye mfuko wa matengenezo ya mara kwa mara, ili hali ya vituo iendelee kuwa nzuri wakati wote.
ReplyDeleteSi haba Masha Allah! Madhali imeshaanza kiulaya ulaya, basi naamini taratibu taratibu hatimae tutafika. Hata Roma haikujengwa siku moja. Ispokuwa tuache tu ile tabia ya uharibifu usiokuwa na maana nadhani na hiyo faini ya laki tatu inaweza kusaidia kuwatia woga wale wenye tabia ya kuhujumu miundombinu mbali mbali iliyopo nchini.
ReplyDelete