Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni
nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe
cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi
hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia,
anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo
NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na kutwaa kombe.
Akitoa nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.
Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia a ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani safi wapenzi wa soka.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili kushoto)

Sheikh Alhadi akifumua shuti
Mwamuzi wa pambano hilo Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akipuliza kipyenga.
Timu ya viongozi wa dini iliyomenyana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Timu ya soka ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha mashiorika na nchi zao hapa nchini
Waziri Chikawe, viongozi wa Acacia, na wale wa TFF wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...