Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437.
Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina.
Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba.
Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa.
Aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kwamba Wamchague kiongozi muadilifu, Mchapakazi na anaechukia rushwa ambae ataendelea kuwaunganisha watanania wote.
Imam wa Msikiti Khadija Jijini Mwanza Mohammed Awadhi akisoma Ibada ya Quran katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Sheikh Mahamood Khasan akisoma ibada ya kuliombea taifa amani katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...