Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dt John Pombe Magufuli,mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar es salam na Vitongoji vyake,katika uwanja wa Jangwani

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jonhn Pombe akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya jangwani,alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio na hatimae aibuke kinara katika nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi Mkuu.
Nyomi uwanja wa Jangwani likiwa tuliiiii.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar na viunga vyake wakati wa kufunga kampeni za lala salama za Mgombea Urais wa chama hicho.Dkt Magufuli,uliofanyika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa wametulia wakisikiliz Sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya viwanja vya Jangwani.
Sehemu ya umati wa watu
Wananchi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakifutilia mkutano wa kampeni wa CCM .
Sehemu ya maelfu ya wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Jangwani kwenye mkutano wa kampeni za lala salama,ambapo Mwenyekiti wa CCM,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ndiye mgeni rasmi,wakiwemo vingozi mbalimbali wa cma na Taifa kwa ujumla.
Mwenyeiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu MKuu wa chama hicho cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.Pichani kulia ni  Mke wa Mwenyekiti wa CCM,Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli ,kwenye mkutano wa kampeni za lala salama uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. CCM oyeeeeee..Kazi imefanyika... kampeni imepigwa nchi nzima iliyobaki nikuisoma namba

    ReplyDelete
  2. Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Kama mbivu au mbichi au mbovu, tayari zimeshajidhihirisha, kazi kwa wahusika na kama ni bidhaa basi ningesema chaguo ni kwa wateja au wanunuzi wa bidhaa hizo husika khasa kwa kuzingatia ubora, kiwango na utahamni wake. Tunashkuru kampeni zilianza na zimemalizika kwa salama na amani, si haba Alhamdulillah. Kazi ni moja tu sasa kwa imani, nia na moyo mmoja ulio mkunjufu kabisa, kuitumia haki yako ya msingi kumchaguwa halali anaestahili pasina kulazimishwa wala kushawishiwa au kurubuniwa na yeyote au chochote kile. Mola tunakuomba utujaaliye uchaguzi wa amani mwanzo hadi kumalizika kwake, ilinde amani, utulivu na usalama tulionao nchini. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...