Afisa vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Massawe
(aliyesimama) akifuatilia majadiliano ya wawezeshaji kitaifa wakati wa kazi za
kikundi kwenye Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Kanda ya
Ziwa.
Na:
Genofeva Matemu - Maelezo
ILIGUNDULIKA kuwa
ulimwenguni kote na hususan nchini Tanzania, Vijana walio nje ya shule ni
miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa yanayoenea kwa njia ya
ngono, VVU na UKIMWI kwa kutokuwa na taarifa na stadi za kuwaongoza hivyo
kupoteza kundi kubwa la vijana ambalo ni taifa la kesho.
Ufumbuzi wa tatizo
hili umeweza kufanyika kwa kuwapa vijana stadi za maisha zenye upeo mpana wa
maarifa na stadi zinazoweza kuwasaidia vijana kuendana na mazingira shindani
yanayobadilika.
Stadi za maisha ni
moja kati ya mikakati iliyobainika kuleta mabadiliko ya tabia za mtu. Stadi
hizi uhusisha stadi na uwezo wa kujenga tabia njema ili kuepukana na matatizo
yaliyopo katika maisha ya kila siku.
Mkabala wa stadi za
maisha unalenga katika kuendeleza na kukuza stadi zinazoitajika katika mahitaji
ya maisha ya kila siku kama vile mawasiliano, kufanya maamuzi, fikra, kuhimili
mihemko, uthubutu, ujenzi wa kujiamini, kuzuia shinikizo rika pamoja na
mahusiano.
Mkabala huu pia
unashughulikia ukuaji wa mtu ili awe na stadi za kumwezesha kutumia aina zote
za taarifa kuhusiana na masuala kama vile magonjwa ya ngono, VVU na UKIMWI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...