Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
14/10/2015 Wananchi wa mkoa wa Lindi wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea mabadiliko ya kweli katika maisha yao kwani kuna baadhi ya watu hawapendi kufanya kazi huku wakisubiri mabadiliko.
Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Ngunichile na Mbaya vilivyopo katika majimbo ya Nachingwea na Liwale (Pichni)waliohudhuria mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana bila ya kufanya kazi kwani kuna baadhi ya watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni kucheza pool huku wakisubiri mabadiliko.
“Hata katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi ni msingi wa maendeleo, hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako”.
“Ndugu zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna maendeleo”, alisisitiza.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...