Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ambaye anafanyia shughuli zake nchini Marekani , leo alikuwa kwenye kipindi cha Runinga cha The Mboni Show kama mgeni mwalikwa akiiwakilisha PSPF akiwa mmoja wa Balozi wa PSPF akiwakilisha DIASPORA.
Akiwa kwenye kipindi hicho sambamba na mwanadada Mboni Masimba alizungumzia masuala mbalimbali ikiwepo maisha ,familia sambamba na kazi zake kama balozi wa PSPF ndani na nje ya nchi. PSPF ni wadhamini wakuu wa The Mboni Show .
Mara baada ya show hadhira iliyokuwepo ilijiandikisha katika mpango wa kuchangia kwa hiari wa mfuko huu wa PSPF , Ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na mfungo huo ambao zaidi ya kupata mafao pia unaweza kukuwezesha kununua nyumba /viwanja / mkopo kwa wajasiriamali /wa elimu na mengi mengineyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...