Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. Mwenyeez Mungu amlaze pema peponi Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Kambarage Nyerere - AMEN.
    Kwa kweli some people are really 'Prophesied' and I truly I believed Mwalim J.K.Nyerere was one of them. Yote aliyoyaongelea bado ni tatizo kubwa kwa nchi yetu na yasipopatiwa suluhu hadi leo hii, basi yawezekana yakawa ni kikwazo cha kudumu katika harakati nzima za maendeleo ya nchi yetu in all aspects. Kwa hiyo wakati ndio huu sasa wa watanzania kuzinduka na kuamuwa kwa dhati bila mashinikizo na iwe ni kutoka katika mioyo yao na sio kwa mashinikizo ya kutaka kuwaridhisha tu wachache kwa manufaa yao. Hivyo basi ni jukumu letu kumchaguwa atakaetufaa kwa kuridhishwa na utendaji pamoja na uwajibikaji wake kwa jumla tangu huko nyuma, mwenye kujali maslahi ya walio wengi kwa manufaa na faida ya watanzania wote kwa jumla. Mola tusaidie katika hili ili tumpate kiongozi bora na aliye chaguo la wengi ambae tunaeamini kwa dhati ataweza kabisa kuwatokomeza aduwi hawa wa sugu ambao ni Rushwa, Umaskini, Udini na Ukabila na mengineyo ambayo sio khulka wala silka yetu watanzania na nchi nzima kwa jumla. Mungu ibariki Tanzania na watu wake na Africa kwa jumla.

    ReplyDelete
  2. SI MWINGINE BALI NI DKT JOHN POMBE MAGUFULI.
    DR GANGWE BITOZI.

    ReplyDelete
  3. lowasa ajipime na hotuba hii

    ReplyDelete

  4. NEXT PRESIDENT NI DR. POMBE MAGUFULI

    ReplyDelete
  5. Tutizame misingi ya tatizo la Rushwa Tanzania. Mfumo huu ulivyoanza na uwezekano wa wagombea wetu kumudu kupiga vita Rushwa. Tufumue Mfumo ambao umejikita ktk mzizi huu! Tusikate tawi lililokuwa linalishwa na mzizi.

    ReplyDelete
  6. Kwanini uliondoka mapema Mwalimu. Ungekuwepo leo ungeona wagombea wa nafasi za uongozi wanavyo jinadi kimakabila, kiudini na viongozi wa dini wakishabikia, na kiufisadi. Mungu ilinde nchi yetu. Watanzania tuwaombaji kwa mungu hivyo tutapata raisi aliye andaliwa na mungu ili tuendelee kuwa mfano kwa nchi nyingi za ukanda wa afrika mashariki, afrika na dunia nzima. Ameni

    ReplyDelete
  7. Magufuli juu zaidi

    ReplyDelete
  8. Mfumo ni nini jamani;Tuelimishe maana hatuelewi wengine?

    ReplyDelete
  9. mfumo maana yake ni kufumua

    ReplyDelete
  10. Dr John Pombe Magufuli, wewe ndiye Rais wetu, huna mpinzani baba!!! Udumu na Mwenyezi Mungu akubariki!! Mungu Ibariki Tanzania !!!

    ReplyDelete
  11. Mtowa maoni no. 8 hapo juu uliyeomba ufahamishwe 'Mfumo' ni nini. Kwa ufahamu wangu ni muundo au ule muonekano ama mtindo wa kitu au jambo linavyoonekana kuwepo kwake au kutumika, yaani ni ile 'format' in general. Ispokuwa inategemea ni vipi, wapi au kukhusiana na nini au kitu gani neno hilo (mfumo) limetumika. Na kwa kuchangia tu, neno 'kufumua' nadhani linaendana na kitu kilichokuwa kimesukwa, kushonwa ama kufumwa badala yake kikahitajika kuuonekana katika hali yake ya awali, then hapo neno 'fumua/kufumua' ndio pahala pake.

    ReplyDelete
  12. Ankal Asante sana kwa kumbukumbu nzuri sana.Tatizo sasa hivi watu tumeshabadilika.Tunapiga kura kwa 'mahaba' kwa mtu fulani na si kama alivyokuwa anataka Mwalimu.Ni shiidah.That was then and this is now.Kama alivyosema Rais wetu Jakaya Kikwete huko Zanzibar majuzi.Uchaguzi wa mwaka huu ni balaa.Ni uchaguzi mgumu sana.Tena Mr.President alisema kama ungekuwa mpira wa miguu basi uchaguzi wa mwaka huu ni wa MAN TO MAN.Mimi nasema MUNGU IBARIKI TANZANIA.Uchaguzi uoite kwa amani nchi isonge mbele.

    David V

    ReplyDelete
  13. Ankal eeee, kwa kutusaidia sisi wenye masikio ya kenge, hebu endelea kutuwekea hiyo ya Baba, Mwl. mpaka siku tunampata Rais wa awamu ya tano, nae si mwingine ila JEMBE CHAPA YA MAMBA. Watoto wa wakulima watayakumbuka majembe chapa ya Mamba, yalikuwa hayaishi wala hayajikunji hata ukigonga kwenye jiwe, changalawe, ndiyo kwaaanza unalinoa.

    ReplyDelete
  14. HK wewe ni mshabiki....hiyo maana ya mfumo uliyotoa siyo sahii kabisa. Mfumo huwezi kuwa kitu au jambo. Mfumo ni combination ya mambo mengi kuanzia governance (yaani utawala, how we lead the country, jinsi wizara mbalimbali zinavyofanya kazi pamoja kuachieve the common goal),to economics of the country (yaani sera za uchumi zinavyokuwa translated into day to day life).

    Anayesema mfumo unatakiwa kufumuliwa ili tuweze piga hatua mbele kama taifa, yuko sahihi kabisa. Mfumo wa sasa hautupeleki kokote, ndo maana wenzetu wanakimbia sisi tupo tunatambaa.

    Nina wasiwasi na Dr Magufuli kama anaweza kutupeleka tutakako, akiwa ndani ya mfumo uliotufikisha hapa. Kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza another 10 years.....

    Haya ni mawazo yangu tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Magufuli anaweza sana maana ameonyesha kupinga waziwazi na KUONYESHA nia ya kufumua mfumo hii kuriko yule aliondoka kwa kufukuzwa na kujitamba kuwa anachukia mfumo huo,

      Delete
    2. Hatua ya kwanza na ya lazima ya kubadilisha mfumo ni kuweka katiba mpya inayoyokana na maoni ya wananchi. Magufuli pa.oja na CCM yake hawatalifanya hili na hivyo hawafai kabisa kukabidhiwa serikali kwa awamu ya tano

      Delete
  15. Uliyesema HK ni mshabiki.....itakuwa umejibu unavyofaham wewe na hukulenga kilichoulizwa. Mtowa mada aliyeuliza yeye alitaka kufahamishwa tu ni nini maana ya MFUMO na kuomba aelimishwe kwani si kila mmoja mjuwaji wa kila jambo, isitoshe tupo hapa kufahamishana, kurekebishana na kuwekana sawa tena kiustaarabu na siyo kwa jazba au kukurupuka. Nadhani kauliza neno 'mfumo' kwa jumla lina maana gani na ndio maana nikasema kwa ufahamu wangu mie... na ndio maana nikaweka wazi inategemea ni katika mazingira gani, kitu gani au jambo gani neno hilo limetumika. Pia aliyemjibu maana yake ni 'kufumuwa' kwa upeo wangu nimeona hakuwa sahihi ndio maana nimejaribu kutoa maoni yangu binafsi. Sina ushabiki wowote zaidi ya kuiombea amani na salama nchi yangu.

    ReplyDelete
  16. Magufuli Atosha.

    ReplyDelete
  17. Mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi, amin...!Watanzania wanataka mabadiliko naamini tutayapata ndani ya ccm na siyo nje ya ccm, mungu ibariki tz, All the best mr.John pombe magufuli

    ReplyDelete
  18. Baba tuombee nchi uliyoiacha salama ibaki kuwa salama. Mungu utufunulie Rais wa watanzania tumpigie kura ili atuongoze kwa dhati kupambana na rushwa, udini, ukabila na umaskini

    ReplyDelete
  19. Mwalimu ameongea mengi sana - sema kuna tunayopenda kusikiliza na kuna tusiyopenda kusikiliza. Kazi kwako mpiga kura.

    ReplyDelete
  20. Ni muhimu tuchague Rais anayeweza kuthubutu kusimama na kukemea hili suala la rushwa katika upana wake na uzembe kazini.

    ReplyDelete
  21. Mfumo maana yake ni "system " au "package "

    ReplyDelete
  22. 'System'(Mfumo) ni sahihi zaidi kuliko hiyo 'Package' lakini mie naona ni kama umetafsiri tu neno 'Mfumo' kwa lugha ya kiingereza ila bado hujatowa maana yake sahihi au husika. Naweza kusema ni sawa na mtu kuuliza 'mkandarasii' ni nani na akajibiwa Mkandarasi ni 'Engineer' inakuwa bado tumegandia pale pale, sawa na Mama ukamwita Bi Mkubwa.

    ReplyDelete
  23. Mfumo ni muundo wa uendeshaji wa taasisi husika.

    ReplyDelete
  24. Yaonesha huu mfumo ni kama "blackhole", maana kuna walioingia wakiwa waadilifu wametoka wakiwa wamechafuka. Ndio maana inatakikana mfumo wote wa chama tawala ukae pembeni, wakati tunaanza kusuka upya!! Kwa bahati mbaya rekodi hazioneshi kama JPM ana ushawishi wa kutosha ndani ya chama na nguvu za kushughulikia vinara waliousuka huu mfumo! Kumbuka "mfumo" ulimshinda nguvu hata Mwalimu wakati wanalichakachua Azimio la Arusha ili kutoa fursa ya mavuno kwa viongozi!! Na ukifuatilia vizuri, maovu yote makubwa yalikuja baada ya Mwalimu kuondoka Duniani!!

    ReplyDelete
  25. Tuone kama kivuli cha Mwalimu kitawasadia safari hii. Roho zinawauma. Mpo kimasilahi na wala si ki-journalist. Mnajifanya hamjasikia kuondoka kwa Kingunge CCM. Eti mnajifanya siyo habari. Roho inawauma, mtakula wapi bila CCM. Fear of the unknown. Get used to it. Wananchi wamekwishaamua hivyo.

    ReplyDelete
  26. Mfumo wa chama tawala yaani CCM upo safi hauna shaka hata kidogo . Tanzania na watanzania wanahitaji taasisi ya umma isio na sura ya ukanda, CCM ni moja ya taasisi zisizoendekeza ukanda hata kidogo. Kwa hivyo tatizo la CCM si mfumo hata kidogo bali ukosefu wa maadili ya baadhi ya watendaji wake kama akina lowasa na sumaye. Kauli wanazozitoa watumishi hao wa zamani wa serikali ya CCM kwa umma kwamba tangu enzi za Mwalimu nyerere hakuna kilichofanyika ni ushahidi tosha za ukosefu wa kutisha wa maadili wa viongozi hao kwa sababu wanazungumza uongo. Magufuli ni mtu sahihi kabisa kwa wakati huu wa kuiongoza nchi kuliko mtu mwingine yeyote yule. CCM na mfumo wake inaweza kumuajibisha Mr magufuli iwapo ikitokea kufanya makosa makubwa ya kuigharimu nchi lakini chadema ukawa hawata thubutu kumuajibisha lowasa ikitokea kufanya makosa makubwa ya kuigharimu nchi kwa sababu lowasa yupo juu zaidi ya chama yaani lowasa ananguvu kuliko taasisi anayoiongoza hakuna wa kumkemea sasa hiyo ni hatari kwa mtu mwenye mihemko ya kimaamuzi kama lowasa.

    ReplyDelete
  27. Lets call a spade a spade! Rushwa na ufisadi unafanywa na WATU , narudia WATU, hili dubwasha linaitwa mfumo ni namna ya ki-ujanjaujanja ya kusafishana tu! Kuna watu wanatumia sio waadilifu wakipewa madaraka wao wanayatumia vibaya, hawaridhiki wala kuguswa na mambo ya wananchi,tunahitaji mtumishi wa wananchi mzalendo kwelikweli. Tuwakatae wasio waadilifu tar 25!

    ReplyDelete
  28. kwani mwalimu huyo aliempigia debe kipindi hicho mheshiwa mkapa alitekeleza yote hayo?sidhani.

    ReplyDelete
  29. Swali la kujiuliza hapa na linalohitaji jibu makini ni kwa nini watu wanaingia waadilifu wanatoka wachafu? Kama tatizo si mfumo ni nini?

    Eddy.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza kabla ya kukujibu ninapenda kukuambia kuwa hilo jina ulilotumia sio lako.Wewe tunakufahamu siku nyingi na jina lako tunalifahamu sana. Wewe ni mamluki uliyenunuliwa na hao mafisadi papa, pamoja na jamaa zako akina Mbowe na kina Lissu.

      Pili, mafisadi wote papa waliingia wachafu toka mwanzo, ndio maana Mwalimu Nyerere alimkataa Eddy Lowassa siku nyingi kabla hata ya Richmond kutokea. Richmond imetokea miaka mingi baada ya mwalimu Nyerere kufariki. Kwa maana nyingine, ukimpa Eddy Lowassa nchi leo, tutegemee Richmond nyingine.

      Nchi yoyote duniani haichagui chama kuongoza, inachagua Rais, hivyo nasisi bongo tunatakiwa kuchagua Rais sio chama.

      Kwa kuangalia wagombea wote hao, Magufuli pekee mwenye uwezo wa kubadili Tz kwa kuwaweka pembeni mafisadi wote.

      Eddy Lowassa hana ubavu wowote kwa kuwa yeye mwenyewe ndio hao mafisadi papa aliyeweza kuwanunua CHADEMA na UKAWA wote ikabidi waweke katiba yao pembeni na kumpitisha kuwa mgombea pekee.

      Kitu kinachoshangaza ni hawa akina Kingunge na kina Mwapachu, wanadai CCM walikiuka utaratibu wa kumpata mgombea. Je CHADEMA na UKAWA wao walitumia utaratibu au katiba ipi ya kumteua Eddy Lowass kuwa mgombea pekee?

      Delete
  30. Ni vigumu kuwaonglea ambao hawajashika dola dhidi ya walioshika dola kwa miaka Nijuavyo team ambazo huwa wanaziita "underdog" wakati mwingine huwa zinawashangaza wengi kwa kupata ushindi ambao haukutarajiwa. Upinzani siyo wa kuubeza. Kwa wale wenzangu ccm tujue kazi ipo kwenye mchuano wa mwaka huu.

    ReplyDelete
  31. We Anony wa October 16, 2015, kama unajiamini kwa kujenga hoja huna haja ya kumjua mto hoja, wewe jikite kwenye "issue" iliyo mezani, la sivyo utakuwa unaonesha udhaifu katika fani hii kama inavyodhihirishwa na pragraph yako ya kwanza!

    Tukirudi kwenye hoja, hoja kubwa nchi hii inatakiwa kuangalia ni nani anayeweza kuikomboa nchi kutoka katika ahadi hewa zilizopita ambazo zimelifanya taifa kuwa maskini, ombaomba, wananchi kukosa kujiamini, na kuwalipa watu kwa jasho lao! Maana hapa hatuhitaji kugawiwa fedha (kama wanavyosema 50m kwa kila kijiji), ni mfumo utakaomlipa kila mtu kwa jasho lake! Mfano waliowanyanyasa wakulima wa korosho kwa kuwapunja bei ya korosho zao bado wapo wanagombea tena kwa tiketi ya ccm! Ndo hapo unapojiuliza nia ya dhati kwa chama tawala kuondokana na huu ubadhilifu!!

    Tusipoacha unafiki na kujadili hoja muhimu Taifa letu litazidi kudidimia! Tuhumua za Richmond na ushiriki wa ENL, ni moja tu ya tuhuma nyingi sana zinazosababishwa na mfumo duni wa Governance, ambao ulitakiwa kubadilishwa wakati wa mapendekezo ya Warioba. Lakini unafiki unafanya kazi yake baada ya kuona hata Warioba anasimama jukwaa moja na wale waliokanyaga maoni yake, makamu wa kukanyaga hayo maoni akiwa ni mgombea mwenza wa ccm!!

    Ndo maana sioni nia ya dhati kutoka kwa JPM, labda afanbye kama yule rais wa Malawi mara atakapoapishwa, kama akishinda!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka nikupe pole sana kwa kuweweseka, mimi sikuhitaji kufahamu jina lako, ila wewe ukajiandika kuwa na jina la Eddy, ndio sababu nikakueleza kuwa jina hilo sio lako kwa kuwa mimi ninakufahumu sana.

      Ukizungumzia hoja iliyoko mbele yetu, ni dhahiri kabisa kuwa Magufuli ni bora zaidi ya wagombea wote wanaogombea urais. Magufuli kajipanga kisawasawa.

      Ukimsikiliza Magufuli kwa makini mbali na hizo ahadi za sh. 50m kila kijiji, yeye anazungumzia viwanda. Kwa maana nyingine amejipanga kutengeneza ajira nyingi sana kutokana na viwanda. Katika hilo la viwanda pekee litaweza kukuza uchumi wa watanzania mmoja mmoja na nchi yote kwa ujumla. Hiyo bei ya korosho unayoisema, itaongezeka mara dufu mara baada ya viwanda kuanza. Hizo 50m zitawaongezea wakulima vijijini uwezo wa kulima kwa kuwa watakuwa na uhakika wa masoko. Atateua baraza lenye mawaziri waadilifu, ndio maana mafisadi wengi waliokuwa CCM wamemfuata fisadi mwenzao CHADEMA.

      Historia ya Magufuli katika utumishi wake ni ushahidi tosha kuwa atatekeleza kwa uadilifu yale yote aliyoahidi. Kumbuka kuwa bila uadilifu huwezi kufanya jambo lolote la maendeleo, hata nchi zilizoendelea ni kwa sababu ya uadilifu uliokithiri.

      Lowassa hana jipya zaidi ya kuwaza kupiga madili mara tu akiingua Ikulu. Ukimsikiliza kwa makini anasema anachukia sana umaskini, ila haelezi atauondoaje umaskini, zaidi ya kusema elimu,elimu, elimu. Ni kweli elimu ni nzuri sana, lakini kuna wasomi wengi sana bongo ambao hawana ajira, je utawaambia warudi shule tena? Vilevile elimu inahitaji pesa nyingi ili uweze kuifanya bure, na haelezi atapataje pesa za kuwarudisha shule watu wote waliomaliza shule ambao hawana ajira. Hata hivyo wasomi wote waliohitimu masomo yao, hitaji lao ni ajira sio kurudi shule tena.

      Historia ni ushahidi tosha kuwa, ukimpa nchi Lowassa, utegemee Richmond nyingine. Hii imethibitisha pale ambapo amewanunua Chadema na Ukawa, wakaweka katiba yao na utaratibu wao pembeni na wakampa kugombea nafasi ya urais bila mpinzani. Hii imedhihirisha kuwa akiwa rais hakuna atakayeweza kumshauri.

      Pia yakupasa ukumbuke kuwa, Lowassa alianza kupiga madili miaka mingi hata mwl. Nyerere, Lissu, Mbowe, mch. Msigwa, Slaa, Lipumba na wengine wengi waliishamsema miaka mingi, hivyo si rahisi kubadilika.

      Delete
  32. Magufuli ni muarubaini wa matatizo ya nchi kwani wanyonge watanufaika zaidi la kama mnataka kuwanuifa wachache basi mchagueni lowasa.

    ReplyDelete
  33. Mdau kutoka New york city,
    Licha ya kuwa tumehamishia makazi yetu ughaibuni lakini nyumbani ni nyumbani na kila kinachotokea huko nyumbani kinatugusa hasa. Nafiri moja ya jambo mtanzania inabidi ajifunze katika nchi hizi za nje ni kuhusu suala la kuwa mkweli au kuzungumza ukweli bila kumumunya au utaingia matatizoni . Sasa siasa zimekuwa nyingi huko nyumbani kuliko ukweli kiasi kwamba hata ule uwongo umeaminishwa uonekanwe ndio ukweli. Huku kuna msemo wamerikani wanasema usiende kufanya (groceries shopping) manunuzi ya vyakula vya nyumbani wakati unanjaa utanunua hata usicho kihitaji na mwisho wake ni upotevu wa pesa na hasara. Sasa utaona watanzania wanahamu,wananjaa,wanahasira ya kumpata kiongozi atakae waondoshea hali ya matatizo yanayowakabili hasa umasikini lakini licha ya hasira hizo watanzania mfahamu kuwa hasira ni hasara siku zote mtu mwenye kufanya maamuzi ikiwa hasira imemtawala matokeo yake hufanya maamuzi mabovu. Katika kukaa kwangu nje nimeshudia na kushiriki chaguzi kadhaa nimeona jinsi au sifa gani wamerikani inawapelekea kumchagua raisi wao?
    Naweza kusema mara nyingi wenzetu wanaangalia sifa za mgombea kwanza sio chama hilo la kwanza
    La pili record au kumbukumbu za maisha ya mgombea hasa maisha yake binafsi na familia yake na cha msingi zaidi ni kumbukumbu za maisha yake ya kazi ya mgombea husika.
    La tatu ambalo naweza kusema limebeba yote hayo ya juu ni uadilifu kwani baada ya sifa zote mgombea atakazokuwa nazo wenzetu hukaa chini na kujiuliza vipi uadilifu wa mgombea hapo mgombea hatakiwi kuwa na kashifa ya aina yeyote . Na kama mgombea anahusika na kashfa hata ikiwa ndogo kiasi gani basi sio kugombea uraisi bali mtu huyo siasa kwake ataziangalia kwenye tv hasubutu hata kukanyaga kwenye viwanja vya siasa kwani hapa watu wa sisa hawataki kusapotiwa na watu wenye makashfa.
    Kwa hivyo tumeona huko nyumbani kuna miradi sana ya kimaendeleo imeanzishwa. Kama bandari kubwa ya bagamoyo.
    Barbara za juu Daresalam.
    Ujenzi wa kiwanda kitakacho jihusisha na uchimbaji wa chuma pamoja na viwanda vitakavyo jihusisha na uchimbaji wa gas.
    Kwakweli hiyo miradi ni mikubwa kwa Tanzania na hatima ya Tanzania kutoka ipo hapo.
    Kwa hivyo maombi yetu kwa ndugu zetu bila ushabiki tunakuombeni mchagueni mtu sahii mwenye uwezo wa kazi wa kusimamia hiyo miradiili bila ya kujali chama chake ili akutoeni kimaisha ama sivyo mtakuja kujuta baadae.

    ReplyDelete
  34. OOh, mimi nikiwa presidaa nitamtoa nanihii kule jela, aaah jamani hii nayo ni sera.

    ReplyDelete
  35. Watanzania tuache ushabiki maandazi. Magufuli ni suluhisho, hata akiongea unaiona kweli ndani yake, bora mama Anna pia lkn sio hao wengine. Unaulizwa swali utaondoaje ufisadi unasema ukasome kwanza Ripti? Eti unaweka bondi gesi ili upate mkopo! Really???? Unataka Urais hujui mipango??

    ReplyDelete
  36. mpende msipende na mtake msitake, Magufuli atosha!! Tz mkimchagua huyo Lowassa mjue mmekwisha nchi mmeikabidhi mafisadi!!
    chagua magufuli chagua maendeleo!!
    mdau wa UK

    ReplyDelete
  37. The mdudu, ndoto ndoto ndoto zitaniuwa ndoto 3 nimeziota Leo Leo ndugu zangu watanzania kwa yoyote anae nifuatilia hapa kwa Mjomba Michuzi nilisusa hata ku comment ila baada ya kuota naludi tena ndoto ya kwanza kwanini wale wametoka CCM? Jibu ndio waliokua wanamfanyia makusudi rais Kikwete ili achemshe na waje kupata la kusema so mambo yote yaliotokea ya UFISADI ni mipango mahususi kupitia wafanyakazi wa idara zote za serikali na ndoto ya 2 kwanini wameenda upinzani? jibu ili watimize ndoto zao lakini ndoto ya 3 watanzania wata mchagua nani siku ya Jumapili jibu ni MAGUFULI tena kwa kishindo lakini wapinzani watasema ha kushinda kiharari kwakua mipango yao imeenda kombo.

    ReplyDelete
  38. Siku saa siyo mbali, In Sha Allah tufike kesho,
    Wananchi sikubali, wenye sera za vitisho,
    Siha walodhofu hali, hao wawekeni mwisho!
    JOHN POMBE MAGUFULI, ndo la peke suluhisho.

    'HAPA KAZI TU'



    ReplyDelete
  39. kura yangu nampa magufuli(namwamini sana magufuli nampa kura kwa moyo mweupe) ...na ya ubunge nampa hassanali(zungu hana jipya sikuona cha maana apumzike kwanza )..na ya udiwani nawapa ukawa pia....lowasa uraisi utausikia kwenye redio..

    ReplyDelete
  40. https://www.youtube.com/watch?v=pGq8KulVrEk
    or
    https://www.youtube.com/watch?v=fvkWbhmYYxU

    Bila shaka alikuwa sahihi

    ReplyDelete
  41. uadilifu uliotukuka sio uliokihili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...