Home
Unlabelled
I SHOT BI KIDUDE - OFFICIAL TRAILER - Maisha Ya Bi Kidude - filamu mpya na Andy Jones
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Awasome! Hii safi.
ReplyDeleteMasha Allah. Mwenyeez Mungu mraham na umughufirie kwa yote mpumzishe pema peponi anapostahili-AMEEN. Kweli marehem Bi Kidude a.k.a. Bi Fatuma Binti Baraka. Kusema kweli alikuwa ni mchango mkubwa kwa Taifa japokuwa naweza kusema alikuwa ni mithli ya hazina iliyofichika au kufutikwa pasina kuidhihirisha thamani yake kwa mujibu wa ilivyostahili kwa kipindi kirefu sana mpaka miaka hii hivi karibuni. Kwa kweli hakuna alokuwa hamfaham Bi Kidude, khususan kwa wakazi wa kisiwani Unguja na khasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Alikuwa mcheshi na mtu wa bashasha kwa rika zote, kwa aliyemfaham na asiyemfaham, almuradi tu umebahatika kukumbana nae uso kwa macho. Mbali ya hilo, mchango wake mkubwa kisanaa na khasa katika fani hii ya muziki wa taarab utaendelea kukumbukwa sasa na hata kwa vizazi vijavyo. Binafsi nimemfaham Bi Kidude tangu utoto wangu kwani ilikuwa hukosi kumuona kila unapopita mitaa ya rahaleo, alikuwa haadimiki au utamuona kakaa barazani kwake, na kwa enzi hizo alikuwa hakosekani kusikika au kuwepo kila palipokuwa na shughuli (harusi) ambapo ngoma yake ya 'Unyago' itakuwepo. Kweli katuachia pengo kubwa na naamini pengine tulikuwa na tashwishwi ya kutaka kufaham au kuyaskia mengi yakhusuyo historia yake kwa undani zaidi na mapitio ya maisha yake, lakini haikuwa rizki, Mwenyeez Mungu kapitisha rehma yake. Pumzika kwa amani Marehem Bi Fatuma Binti Baraka almaarufu Bi Kidude - A M E N.
ReplyDeleteKwa hamu tunaisubiri hiyo filamu mpya ikhusuyo Maisha Ya Bi Kidude. Natanguliza shukran na pongezi za dhati kwa waandaaji na wote waliohusika katika kulifanikisha hilo.