Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015
Tunakupongeza mheshimiwa rais mteule Magufuli, hongera rais wa awamu ya tano mtarajiwa.
ReplyDeleteTunamshukuru Mungu kwa kutufikisha hatua ya kumaliza mchakato wa kuchagua viongozi wetu kwa amani na kuwapongeza wote waliochaguliwa na kushiriki katika mchakato huu.
Tunakuombea Mungu rais mteule akupatie hekima unapochukua jukumu hili muhimu la kuongoza nchi hii wewe pamoja na wote watakaokusaidia katika uongozi wa taasisi mbalimbali.
HONGERA MHESHIMIWA. HONGERA WATANZANIA. MUNGU IBARIKI TANZANIA
mhhhhhh
ReplyDeleteHongera Rais wetu mteule tunakutakia mafanikio katika awamu ya tano. Tanzania Oyeeee, CCM na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi Oyeee tuungane kumuunga mkono rais wetu wa awamu ya tano.
ReplyDeleteWote waliofanikisha uchaguzi huu kwa njia moja au nyingine tunawapongeza sana sasa tuna madiwani na wabunge na pia rais mteule. Asante Tume ya Uchaguzi kwa kazi kubwa, nchi hii kubwa mmefanya kazi kubwa. Hongera Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa kujitahidi kufanya kazi nzuri ya usalama nchini. Wakuu wa wilaya na mikoa kwa kazi nzuri. Uchaguzi wa bara umeisha kwa sehemu kubwa. HAPA NI KAZI TU inaanza tushirikiane kuleta mabadiliko.
Hongera Rais Mteule, namba tumeisoma, wengi wamepewa, jukumu lako ni kutupenda wote tuwe CHAUMA, UKAWA, ACT, nk.
Tushirikiane kuendeleza nchi hii.
CONGRATULATIONS
ReplyDeleteCongratulations are also due to all peace loving wananchi. Wale ambao hawakubaliani na matokeo hayo, wana haki zao zinazotambuliwa na sheria na mahakama. Sisi hatutaki fujo tu. Mungu ibariki Tanzania.
Congratulations Your Excellency John Magufuli for winning this election as a country we celebrate with you and your party CCM on this achievement.
ReplyDeleteWe wish you all the best as you assume the responsibility of being the Fifth head of state of our beautiful country the United Republic of Tanzania.
We are looking forward to better governance at all levels and to make significant strides in development at all levels.
May God bless our country and people.
Congratulations.
Hongera Dr Magufuli and Shukran sana Mhe Rais Kikwete kwa kusimamia transition ya uwazi na iliyoimarisha demokrasia nchini kwetu. Mungu akujalie na kukubariki sana.
ReplyDeletePongezi kwako Rais wetu wa awamu ya 5 JOHN POMBE MAGUFULI mimi ni Chadema lakini penye ukweli lazima niseme sisi wenyewe Chadema ndio tumejitakia Chadema bila ya Dr Slaa nilijua tu hakuna ushindi na kibaya zaidi kuna majimbo baada ya kusimama kama Ukawa lakini tumesimama kivyama vyama yaani Chadema na Cuf hili ni kosa kubwa tumejitakia na wala tusimtafute mchawi hapa mchawi ni wenyewe kwa wenyewe so kama kutakua na kuhama sishana eti tuandamane mimi kama mtanzania na mpenda amani sito andamana kamwe na sipendi kuona nawapa usumbufu WATOTO, MAMA ZANGU, BABU ZANGU na DADA ZANGU na Watanzania wote kwa ujumla Asanteni sana ni hayo tu kwa Leo
ReplyDeleteTupo jamaa wengi hapa hatuna uanachama katika chama chochote cha siasa, lakini tunajua wapi Mlima Kilimanjaro ulipo. HONGERA SANA JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
ReplyDeleteSimba wa Afrika
ReplyDeleteCONGRATULATIONS mheshimiwa KIKWETE.
ReplyDeleteThis is an example of our commitment to democracy as opposed to those who talk the talk and do precious little more na kung'anga'nia madaraka by hook or crook.Mungu ibariki Tanzania.
HONGERA SANA SANA SANA Mh. John Pombe MAGUFULI. Mwenyeez Mungu akulinde, akujaaliye afya njema, akuepushe na mabaya yoooote, akujaaliye kila lenye kheri katika utendaji wako mithli na zaidi ya ulivyowajibika na kuwa muaminifu huko nyuma ulipoanzia, akujaaliye moyo wa subira na stahmala popote pale utakapokabiliana na changamoto zozote zile kiutendaji na kiuwajibikaji na akujaaliye suluhisho na ufumbuzi wa salama na amani, akujaaliye upendo kwa wananchi wako nje na ndani, Afrika na dunia kwa jumla, In Sha Allah - AMEN.
ReplyDeleteKwa upinzani pia niwapongeze kwa kuonyesha ushirikiano wa pamoja katika zoezi hili zima la Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania. Mmekuwa watulivu na kuungana pamoja japokuwa tofauti au itikadi za kisiasa huwa hazikosekani, lakini pia hazikuwa chambo au kigezo cha kusababisha ghasia au vurumai nchini, tumekwenda mguu kwa mguu mpaka kutangazwa kwa matokeo na naamini changamoto kadhaa zilizojitokeza ni chache na ni za kawaida ambazo suluhuhisho pia litapatikana tu huku tukiendelea kuwa watulivu na wenye imani na nchi yetu na watendaji husika kwa jumla. Mbali ya hayo, kadhalika tusisahau kuwa sisi ni wamoja na uchaguzi umeshamalizika, hivyo tuendelee na maisha yetu mpaya baada ya uchaguzi na kuungana kama kawaida pasina kuwekeana chuki, hasama wala vinyongo kwa kisingizio cha siasa, tuone ni mithli ya mpira tumeutizama, mshindi kabainika na umeisha tumetawanyika kila mmoja na njia yake kwa salama amani kabisa, huku tukiendelea kushirikiana in all aspects katika maisha yetu ya kila siku. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake, Ibariki Afrika na Ubariki ulimwengu mzima - AMEN.
Kidugu CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!!!!!!!!!!!
Tumejipanga mwaka huu wataisomaaaaaaaa,na wameisoma kweli, wacha wacha jamani raha, jamani raha. uwiiiiiiii. HONGERA MHESHIMIWA RAIS, HONGERA SAAAANA. KAZI KUBWA ILIYOBAKI NAKUSIHI SANA TIMIZA AHADI ZA WATANZANIA. ILI 2020 WAPINZANI WASOME UPEPO SIO NAMBA TENA. HONGEEEEEEEEERA.
ReplyDeleteHongera Sana Rais Mteule Dr John Joseph Pombe Magufuli kwa ushindi wa KISHINDO. Ni dhahiri kuwa yametimia yale yote uliyokuwa unayanena kwenye safari ndefu ya kuwaambia watanzania wote nchi nzima, kuwa WEWE ndo chaguo SAHIHI la kuwa Rais wa awamu ya TANO. HONGERA SANA.
ReplyDeleteNasi wananchi wote, bila kujali itikadi zetu za kivyama, dini zetu, nakadhalika, tuungane na Mheshimiwa Rais Mteule, kulijenga Taifa letu tukufu la TANZANIA, kwa kuchapapa KAZI. HAPA SASA IWE NI KAZI TUUUUUUU...si vinginevyo. Yeyote awaye yule, kama anadalili za UVIVU aanze kuziacha mara moja. Hii ni awau ya KAZI TUUUU. TUNAWEZA, TUMEDHAMIRIA SASA TUCHAPE KAZI.
Kwa vyama vya upinzani: CHADEMA (UKAWA, CHAUMA, ACT, na wengineo, mbio za uchaguzi zimeisha. Changamoto kubwa mliionesha CCM kwa kuchagiza mbio za kuelekea uchaguzi mkuu. Ni kwa mbio zenu tuu, zilipelekea CCM nao kuongeza kasi ya kukimbiza uwigo wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi kwa nguvu zote. Hivyo, nanyi mnastahiri PONGEZI kubwa Sana. Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Uchaguzi umeisha, sasa sote TUUNGANE na TUCHAPE KAZI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA-DAIMA..AMINA!!!
WEWE MTOA COMMENT NAMBA 2 HAPO JUU
ReplyDelete........................
Anonymous Anonymous said...
mhhhhhh
October 29, 2015
........................
mhhhhhh NINI SASA WEWE ULITAKA IWEJE?
WATU WA NAMNA HII NDIO WANAO HATARISHA AMANI NCHINI, NDIO HAWA WANAOJENGA MASHAKA NA MCHAKATO WA UCHAGUZI HADI KUTOA MATOKEO. NA NDIO HAWAHAWA WANAOKAMATWA KWA KUTOA TAARIFA ZA UPOTOISHAJI NA MWISHOWE WANAKAMATWA NA KUWEKWA KTK VYOMBO VYA SHERIA.
SASA KAMA JUMUIYA YA KIMATAIFA NA WAANGALIZI WA KIMATAIFA WENYE UJUZI ZAIDI YETU WAMESEMA UCHAGUZI NI HALALI WEWE UNA SHAKA GANI?
Hongera sana mheshimiwa rais mteule kwa ushindi wa kutosha na pole na mapunziko mema rais mstaafu.
ReplyDeleteUshauri wangu rais mpya fanya Kama ulivyohadi kwenye kampeni zako kwanza wachukilwe hatua wale wote waliolitumbukiza taifa kwenye majanga kwa kuiba pesa za umma na wao kujirimbizia Mali na kuwaacha wananchi wa kawaida wakiteseka kwa kukosa huduma za msingi sina haja ya kukusisitiza sana juu ya hilo watanzani wameipa CCM nafasi ya mwisho na wamekupa imani kubwa kwako kuzitekeleza ahadi sisi wengine ni viona mbali tunaona kile wengine awakioni.
Mh Magufuli ni jembe, na amekuwa jembe kipindi chote cha uwaziri. Nakutakia afya njema Katika kipindi chote cha uongozi wako.
ReplyDelete