RAIS Jakaya Kikwete, akitoa hotuba kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la kitegauchumi PPF Plaza eneo la Vigaeni, mjini Mtwara, Oktoba 10, 2015. Jengo hilo la ghorofa  mali ya PPF litagharimu shilingi Bilioni 9.5 ujenzi wake utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu.

NA K-VIS MEDIA, MTWARA
RAIS Jakaya Kikwete ameumwagia sifa kemkem Mfuko wa Pensehni wa PPF, kwa uwekezaji bora, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jingo la ghrorofatano  la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.
“Nimefurahishwa sana na uwekezaji wenu kwani ninaenda kustaafu na kupumzika kwa raha kutokana na mambo makubwa mliyotafanya, nah ii ni fursa nzuri kwa uwekezaji kwenye mkoa huu ambao utakuwa kitovu cha uchumi.” Alifafanua Rais.
Rais Kikwete, ambaye alitua mkoani humo akitokea nchi I Msumbiji alikokwenda kuaga, alisema, Mtwara yuko muwekezaji ambaye ni tajiri mkubwa barani Afrika akishikilia namba moja, nay eye angependa walau kulala mkoani Mtwara wakati wa ziara zake za kukagua miradi yake, na lakini atalala wapi, wakati hakuna hoteli yenye hadhi yake.? Aliuliza na kuwataka wawekezaji zaidi katika eneo la mahoteli ili kuweza kuwapokea wafanyabiashara wakubwa wanaotembelea Mtwara ivi sasa.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Aggrey Mlimuka, alisema, jingo hilo litakapokamilika ujenzi wake litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 na tayari baadhi ya ghorofa zimeshachukuliwa. Rais Jakaya Kikwete, (katikati), akipunga mkono kuwaaga wafanyakazi wa PPF na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko huo “PPF PLAZA” baada ya kuweka jiwe la msingi.
Rais Kikwete, na Mama Salma Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Waziri wa Nishati, George Simbachawene, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, Wafanyakazi wa PPF, na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara leo Oktoba 10, 2015. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Sad).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...