JAMHURI YA MUUNGANO WA  TANZANIA
                                         MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. 
Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.
Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-

16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui   atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana.  uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   usahihi wa matokeo yote   yanayotangazwa.
16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na  ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.
Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 25/10/2015    
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. ….asanteni, asanteni, asanteni…..
    Wananchi wote asanteni sana kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuchangia na kushiriki katika kuijenga na kuiimarisha demokrasia yetu. Shukurani kwa viongozi wote wa pande zote kwa kazi njema mliyoifanya, sasa wananchi wakotayari kufanya kazi ya kimaendeleo. Kwakweli wananchi wote NA HASA WALE AMBAO HAMKUNIPA KURA ZENU nasema, nchi nzima imeshinda, wote tummeshinda, kwasababu ushindi huu wa #hapakazitu, ni ushindi kwa maendeleo zaidi ya nchi yetu. {makofi, vigelegele, shangilia} LAKINI SASA, KUANZIA SASA, mimi NINAWAONGOZA. NDIO KIONGOZI WENU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. JIUNGENI NAMI….TUIJENGE NA KUIENDELEZA NCHI YETU….

    ReplyDelete
  2. Kwa nini Tanzania inazuiliwa EXIT POLLl{matokeo real jinsi watu walivyo piga kura mara watokapo vituo vya kupigia kura na hutangazwa na vyombo vya habari baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa rasmi}
    Nchi yingi zilizoendelea na zinazoendelea inaruhusiwa na nara nyingi huwa hayatofauti sana na matokeo rasmi yakitoka.
    Mimi binafsi na wabongo wengine wanasubiri kwa hamu kujua matokeo... too long to wait for 3 to 4 days for a result

    ReplyDelete
  3. hhahahahaha mdau wa pili huna habari weye???aha kalagabao

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili hapo juu wewe unaishi dunia gani? Kila nchi ina utaratibu wake yakhe. Ndiyo maana kungine wanatumia ngamia, wengine farasi, wengine mikokoteni, wengine punda na wengine pekupeku.

    Tuache na sisi tufanye ki-vyetu.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 3 na 4 hapo juu bakieni tu hapo mlipo, kwani kinachohitajika hapa ni upesi wa kujua habari mhimu mbalimbali pamoja na hii ya uchaguzi wa rais.
    Utumie ngamia, farasi, mikokoteni, punda swala linabakia palepale kufika haraka huko uendako.
    Kufanya ki-vyetu ni vizuri,lakini lazima tuchague mazuri yafanyavyo na wengine na tuyafanye.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa tatu, uchambuzi wako wa mambo unatia mashaka upanuzi wa demokrasia unaendana na uwazi katika voting process hadi kwenye utangazaji matokeo. Sasa ni vyema tuendelee kutumia bajaji, bodaboda, na mikokoteni wakati wenzetu wanatumia train za umeme ccm oyeee!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...