Na Hassan Hamad, OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amepiga kura katika kituo cha Garagara Shehia ya Mtoni Kidatu jimbo la Mtopepo. Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, amepiga kura katika kituo hicho mnamo majira ya saa nne asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura, Maalim Seif amesema ameridhishwa na jinsi wananchi walivyojitokeza kupiga kura, sambamba na utulivu uliokuwepo katika kituo hicho.
Ameelezea matumaini yake ya kupata ushindi katika uchaguzi huo, na kwamba iwapo uchaguzi utafanyika katika hali ya uhuru, haki na uwazi atakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo.
![]() |
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Garagara kwa ajili ya kupiga kura. |
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa karatasi za kupigia kura tayari kwa kwenda kupiga kura
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura kwenye sanduku la kura.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo. Picha na OMKR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...